Serikali yaunganisha mifumo ya kielektroniki utoaji leseni katika Sekta ya Utalii

NA MWANDISHI WETU

SERIKALI kupitia Wizara ya Maliasili na Utalii imesema imeunganisha mifumo ya utoaji leseni katika Sekta ya Utalii kupitia mfumo wa kieletroniki wa MNRT – Portal kwa lengo la kuongeza tija katika utoaji wa huduma na kurahisisha mchakato wa utoaji wa leseni za biashara za utalii.
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Mary Masanja (Mb) amesema hayo leo Bungeni jijini Dodoma alipokuwa akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalum, Mhe. Cecilia Paresso aliyetaka kujua mpango wa Serikali wa kuunganisha mifumo ya utoaji wa leseni katika sekta ya utalii ili kurahisisha upatikanaji wa leseni.

Ameongeza kuwa hatua hiyo imepunguza gharama, muda na kuongeza wigo wa ushiriki wa wananchi na wawekezaji mbalimbali katika biashara za utalii.

Aidha, kuhusu uhai wa leseni ya biashara za utalii kuendana na kalenda ya Serikali, Mhe. Masanja amefafanua kuwa Serikali imeshaanza kupokea maoni kutoka kwa wadau mbalimbali hususan wadau wa masuala ya utalii kuangalia endapo kanuni za leseni hizo zikipitiwa upya zitaleta tija katika utoaji wa leseni.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news