Simba SC mguu sawa kuivaa Ihefu FC leo

NA DIRAMAKINI

WEKUNDU wa Msimbazi (Simba SC) ya jijini Dar es Salaam leo wataingia dimbani katika mtanange wa Robo Fainali ya Azam Sports Federation Cup (ASFC) dhidi ya Ihefu FC.

Ni mtanage ambao utapuigwa leo saa moja usiku katika Dimba la Azam Complex lililopo Kata ya Chamazi Halmashauri ya Manispaa ya Temeke jijini Dar es Salaam.

Awali mchezo huo ulipangwa na kutangazwa kuwa utafanyika saa 10 jioni katika dimba hilo hilo la Azam Complex, lakini muda huo umebadilishwa na sasa utapigwa usiku.

Maamuzi ya kusogeza muda mbele ni kuwapa nafasi mashabiki waliopo kwenye Mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani kufuturu na wale Wakristo kufanya ibada ya Ijumaa Kuu.

Mchezo huo utakuwa ni wa kwanza kwa Simba kucheza katika Uwanja wa Azam Complex msimu huu kufuatia ukarabati unaoendelea katika Uwanja wa Benjamin Mkapa uliopo Halmashauri ya Manispaa ya Temeke jijini Dar es Salaam anbao huwa wanautumia kwa mechi za nyumbani.

Kocha Mkuu, Roberto Oliveira ‘Robertinho’ akizungumzia mchezo huo amesema, ni mchezo muhimu ambao wanapaswa kushinda ili kuingia hatua ya nusu fainali na kila mmoja ndani ya timu analifahamu hilo.

"Tunahitaji kucheza vizuri na kupata ushindi utakaotupeleka nusu fainali. Tunajua tunaenda kukutana na timu ngumu, lakini tumejipanga.

“Tumetoka kucheza mechi ngumu ya Ligi ya Mabingwa, lakini hii pia ni muhimu kwetu tunahitaji kucheza vizuri tukiwa na mpira na tusipokuwa nao na kupata ushindi,”amesema Robertinho.

Robertinho amewaomba mashabiki kujitojeza kwa wingi uwanjani ili kuipa sapoti timu kwa kuwa wana mchango mkubwa kwa timu kupata ushindi.

“Mashabiki ni muhimu katika mchezo wa mpira, uwepo wao uwanjani unaongeza chachu na hamasa kwa wachezaji, tunawaomba waje kwa wingi kesho, tuna mchezo muhimu,” amesema Kocha Mkuu huyo.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news