Simba SC yasema lazima Wydad wakae

NA DIRAMAKINI

KIKOSI cha Klabu ya Simba kimeingia kambini jana asubuhi kujiandaa na mchezo wa Robo Fainali Ligi ya Mabingwa barani Afrika dhidi ya Wydad Casablanca kutoka Morocco.

Mtanage huo utapigwa Jumamosi hii katika dimba la Benjamin Mkapa lililopo Halmashauri ya Manispaa ya Temeke jijini Dar es Salaam saa 10 badala ya saa moja usiku kama ilivyozoeleka katika hatua ya makundi kwa kuwa itakuwa ni sikukuu ya Eid El Fitr.

Baada ya mchezo wa Ligi Kuu ya NBC dhidi ya Yanga, Jumamosi iliyopita wachezaji walipewa mapumziko kabla ya kuingia kambini moja kwa moja.

Meneja Habari na Mawasiliano, Ahmed Ally amesema wachezaji wawili Sadio Kanoute ambaye hakuonekana katika mechi kadhaa zilizopita kutokana na majeruhi pamoja na Aishi Manula nao watafanyiwa vipimo.

“Sadio alipata maumivu ya nyonga na leo atafanyiwa vipimo kama itaonekana yupo fiti ataanza mazoezi pamoja na wenzake kama ilivyo kwa mlinda mlango Manula kwahiyo itategemea majibu ya vipimo ili kujua kama wawili hawa watakuwa sehemu ya kikosi,” amesema Ahmed.

Wakati huo huo, hamasa kwa ajili ya mtanage huo imeendelea ambapo kikosi kazi kipo Chalinze mkoani Pwani kwenye uzinduzi wa hamasa kuelekea mechi ya Wydad.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news