NA WILLIAM BOMBOM
Ilipoishia... aliendelea kumlamba kwa kasi huku mtoto akiwa kabanwa hana uwezo wa kuchomoka. Mate ya joka hilo yalikuwa yanateleza mithili ya mlenda wa Kinyamwezi...
Endelea
Padri alikuwa kadhamiria kummeza mzima mzima mtoto huyo, lengo la Padri huyo ilikuwa ni kumiliki hirizi hiyo. Licha ya kuzidiwa ujanja na yule ndege mweusi aliyeichukua hirizi na kumlisha mtoto THE BOMBOM.

Bado Padri huyo alikuwa akiamini kuwa, umiliki wa hirizi hiyo ulikuwa mikononi mwake. Njia pekee ya kuipata hirizi hiyo ni kummeza mzima mzima mtoto huyo, hii ingemrahisishia kuibakiza tumboni mwake. Ndugu msomaji, Padri huyo akiwa kwenye umbo la joka aliendelea kumlamba zaidi mtoto THE BOMBOM.
Mtoto huyo alikuwa katulia tuli mithili ya mbuzi aliyekamatwa na chatu, licha ya kuimeza ile hirizi ya bibi yake, lakini alikuwa chini ya utawala wa Padri.
Kitu pekee alichokuwa akikifanya ni kuomba mizimu ya mababu zake pamoja na mahoka. Hatimaye maombi yake yalifika mbele za mizimu hiyo, ghafla kulitokea kimbunga cha ajabu ajabu.
Kimbunga hicho kilizidi kuongezeka kadri muda ulivyokuwa ukisonga mbele. Kimbunga hicho kilianzia kwenye mashamba ya shule, baada ya muda mfupi kilifika maeneo ya shule. Madarasa ya shule hiyo yalisukwa sukwa kwa upepo mkali, hatimaye kimbunga hicho kilifika kwenye uwanja wa shule.
Eneo hilo ndipo sherehe ya kichawi ilipofanyika, kulikuwa na idadi kubwa ya wachawi waliokuwa wamekufa. Vifo hivyo vilisababishwa na sumu kali iliyotiwa ndani ya chakula walichokula kwenye sherehe.
Kulikuwa na kundi jingine la wachawi waliokuwa wakiendelea na majukumu yao maeneo hayo. Ikumbukwe kuwa kundi la Ng'wana Michembe lilikuwa limeungana na kundi la Padri Samson Mcjohn.
Kundi hilo halikuona umuhimu wa kuendelea kupingana na Padri ilihali kiongozi wao alikuwa ameuawa. Waliungana na kuwa kitu kimoja, walitii maelekezo ya Padri kila walipoamrishwa.
Kile kimbunga kiliendelea kuongezeka kila muda kilipokuwa kikisogea eneo palipokuwa na lile joka na mtoto THE BOMBOM.
Kilipofika eneo husika kilizunguka kwa kasi ya ajabu, mchanga, vumbi, uchafu, nyasi na takataka zingine zilienea eneo zima.
Lile joka likawa halioni vyema, vumbi na mchanga viliingia machoni mwake. Liliamua kumuachia mtoto huyo kisha likajibadili na kurudi katika umbo lake halisi.
Lilikuwa limebaini kuwa kile hakikuwa kimbunga cha kawaida bali kilikuwa cha kutengeneza. Wakati joka hilo likiwa kwenye harakati za kujigeuza, kile kimbunga kilimnyakuwa mtoto THE BOMBOM na kuondoka naye.
Kitendo hicho kilimuudhi sana yule Padri, hata hivyo alijitahidi kupambana ili angalau amrudishe mikononi mwake lakini haikuwezekana. Kisha kile kimbunga kiliyeyuka mithili ya barafu kwenye joto.
Asiyekubali kushindwa si mashindani, huu ulikuwa ni msemo walioutumia mababu. Kwa upande wa wachawi msemo huu hautumiki hata kidogo, ni kosa kubwa sana kukubali kushindwa.
Mchawi lazima apambane hadi tone la mwisho, unapokubali kushindwa ni kukaribisha kifo kwa upande wako. Padri huyo aliondoka eneo alilokuwa na kuelekea palipokuwa na wasaidizi wake.
Idadi ya wachawi waliokufa ilikuwa ni kubwa sana, wasingeweza kuwaacha kiwanjani wakaozea hapo. Yule Padri aliwasogelea maiti hao na kuwatemea mate, kila aliyetemewa mate alipotea maeneo hayo.
Wakati huo walikuwa wameshawanyofoa mioyo, ndimi, sehemu za siri na vitovu. Walichukua sehemu hizo kama vizimba vya kuchanganyia dawa zingine za kichawi, kila mchawi aliyekuwa eneo hilo alikubaliwa kuchukua kizimba kingine alichoona ni muhimu katika dawa zake.
Ndugu msomaji hapa niseme kidogo, mchawi yeyote huwa amezindika dawa sehemu mbalimbali za mwili wake. Huzindika kivuli maana mtu anaweza kukitumia kivuli chako kukuloga, pia huzindika ulimi, miguu, mikono, vidole nk.
Ndiyo maana anaweza kusonta huku akinuia jambo fulani likatokea, ama akatema mate yake kikatokea kitu cha ajabu. Hii huwa ni nguvu ya dawa zilizoko mwilini mwake, ndiyo maana Padri huyo alikuwa akitema mate na maiti zile zinapotea.
Walipomaliza kazi hiyo waliamua kusambaa na kurudi makwao, tayari ilikuwa imetimia saa tisa kamili usiku. Kabla ya kutawanyika, walikaa kitako wakakubaliana kutangaza vita dhidi ya mtoto THE BOMBOM na aliyemuokoa.
Rasmi Padri Samson Mcjohn akawa ametangazwa kuwa kiongozi mkuu wa wachawi kanda yote ya Magu na eneo dogo la Simiyu.
Ndugu msomaji, ndiyo kwanza Padri ametawazwa kuwa kiongozi wa wachawi wa eneo hilo unadhani nini kitampata? Endelea kufuatilia kisa hiki cha kusisimua sehemu inayofuata.
NAHENE