NA WILLIAM BOMBOM
Ilipoishia...yule mheshimiwa kutoka wilayani macho yakamtoka kodo, alijipapasa mfukoni mwake haraka haraka. Lengo lake ilikuwa ni kutoa bastola, alikuwa amedhamiria kumshindilia risasi za kichwa mtoto huyo afie mbali.
Endelea
Mara nyingi viongozi wa ovyo huwa hawana uwezo wa kujenga hoja dhidi ya washindani wao, hupenda kukatisha maisha ya watu kama njia za kujilinda na mambo yao ya ovyo.

Mheshimiwa yule kutoka wilayani, ni miongoni mwa viongozi wa namna hiyo. Alifanikiwa kuichukuwa bastola hiyo iliyonunuliwa kwa kodi za wananchi masikini, akiwa amedhamiria kumfyekelea mbali mtoto THE BOMBOM.
Lakini kabla hajafanya jambo lolote mtoto THE BOMBOM alimuwahi na kumsihi, "Mheshimiwa wangu nimekuambia mie ni nabii, hiyo bastola unayotaka kutumia dhidi yangu haitakusaidia kitu hakika hautafanikiwa. Jambo la msingi unalopaswa kulifanya ni kukiri au kukanusha nilichokisema."
Mheshimiwa yule alisimama akiwa na bastola mkononi, alianza kufoka ndani ya kikao hicho huku akiwa ameishika thabiti bastola hiyo.
Alikuwa akibwabwaja maneno kwa kasi mithili ya cherehani iliyokata uzi. "...mkubwa wewe, huu utumbo wako hakuna mtu mwenye akili timamu anayeweza kukusikiliza. Sikubaliani na upuuzi wako wa kutaka kunichafua jina langu, jina hili nimetumia muda mrefu kulijenga ndani ya jamii.
"Kuaminiwa mpaka nikateuliwa nafasi hii si jambo dogo, leo hii kimburu mdogo kama wewe unataka kunichafua...kabisa kimburu mweupe, sali haraka kabla sijafyatua risasi yangu."
Taharuki iliwavaa wajumbe wa kikao hicho, walibaki wakimshangaa mwenyekiti wao juu ya jambo alilokuwa akitaka kulifanya mbele yao.
Badala ya kusimamia ulinzi na usalama ndani ya jamii, alikuwa ameamua kuharibu usalama huo kwa mikono yake. Walimu walibaki wakitetemeka walivyomuona mheshimiwa akiwa na bastola, mbaya zaidi ilikuwa imeelekezwa kwa mtoto THE BOMBOM.
Waliamini dakika chache zilizofuata wasingelimuona mtoto huyo, ingelibaki historia kwa mtoto huyo. Katika maisha yao hawakuwahi kuona mtu ameelekezwa bastola namna hiyo.
Kwa upande wa mkurugenzi na kamanda wa polisi wilaya walikuwa wakimsisitiza mheshimiwa huyo kutofanya uamuzi aliokuwa kaukusudia. Hakukuwa na haja ya kumuua mtoto huyo, wao walimsihi sana mheshimiwa huyo kurudisha bastola ili warudi kwenye maongezi yao.
Kwa upande wa mtoto THE BOMBOM hakuwa na wasiwasi hata kidogo, mbali ya kuelekezwa bastola aliendelea kujiamini aliiona bastola ile kama toi la watoto.
Aliwasisitiza wajumbe wa kikao hicho kumuruhusu mheshimiwa huyo kufanya alilokuwa amekusudia. Ghafla ulisikika mlio wa kutisha ndani ya ofisi hiyo, paaaaaaaaaaa! Ilikuwa ni risasi toka kwenye bastola ya mheshimiwa huyo.
Risasi hiyo ilipita kwenye kifua cha mtoto THE BOMBOM eneo la moyo kisha ikatokea mgongoni. Taharuki zikatawala ndani ya chumba hicho, kwa kuwa mheshimiwa alikuwa mlangoni hakuna aliyefanikiwa kutoka ofisini humo.
Mtoto THE BOMBOM alilaza kifua chake kwenye meza, huku mgongoni damu zikiwa zinachuruzika mfano wa chemichemi ya maji alionekana kupoteza uhai wake.
Chumbani kulikuwa kimya, hakuna aliyejaribu kuzungumza kwani lililokuwa limetokea lilikuwa ni jambo gumu sana. Baada ya dakika mbili toka apigwe risasi mtoto THE BOMBOM, alikohoa na kuanza kucheka huku akisimama.
Hili liliwashangaza watu waliokuwa ndani ya kikao hicho, hakukuwa na damu wala doa lolote mwilini mwake. Mtoto huyo alisogea ukutani akapagusa kwa kidole chake huku akiwa kimya, ghafla ukuta ulibadilika na kuwa mweupe pee!.
Aligusa tena kwa kutumia chanda chake. Kukatokea video ya watu wawili waliokuwa wakizungumza, watu wote ndani ya ofisi hiyo walianza kuifuatilia video hiyo.
Kwa kuwa video hiyo ilikuwa ikitoa sauti, waliweza kufuatilia maongezi ya watu hao. Watu hao wawili alikuwa ni Padri Samson Mcjohn na mheshimiwa kutoka wilayani, walikuwa ofisini kwa mheshimiwa huyo wakizungumza.
Maongezi ya watu hao ilikuwa ni mipango ya namna ya kukwamisha shughuli za mtoto huyo. Pili ilikuwa ni kubuni njia itakayopelekea kuuawa kwa mtoto huyo,mheshimiwa huyo alionekana akiomba rushwa kama ujira wa kazi hiyo.
Aliomba bilioni tano kama alivyokuwa ameeleza mtoto THE BOMBOM kwenye kikao hicho. Katika kikao hicho mambo mengi yalizungumzwa, huku kila mmoja akifuatilia kwa karibu hatua kwa hatua.
Yote haya yalifanyika mbele ya mheshimiwa huyo akijiona, alishangaa kuona siri yake ikiwa imewekwa hadharani. Mheshimiwa huyo alikuwa kijana kwa umri, lakini alikuwa na ukwasi uliowachanganya watu wengine. Kumbe mali zake zilipatikana kupitia madili ya hovyo aliyokuwa akiyafanya.
Mtoto THE BOMBOM aliondoa video hiyo kisha akaleta video nyingine iliyokuwa ikionesha namna mheshimiwa huyo alivyokabidhiwa hundi ya bilioni tatu toka kwa Padri huyo.
Kulikuwa na video nyingi zilizooneshwa ukutani hapo zikionesha maisha kamili ya Padri huyo toka kuzaliwa mpaka kuja Afrika.
Video hizo zilionesha pia shughuli za kichawi zinazofanywa na Padri huyo. Jambo pekee ambalo halikuoneshwa ni uwepo wa mtoto THE BOMBOM kwenye uchawi.
Mambo yalikuwa mengi yaliyowafanya watu ndani ya ofisi hiyo kubaki kinywa wazi. Upepo ulikuwa umebadilika kila mtu alikuwa akimuamini mtoto huyo, waliamini kabisa mtoto huyo alikuwa ni nabii aliyetumwa na Mungu.
Hakuna aliyejua kuwa mtoto huyo alikuwa nabii wa kichawi, ndiyo maana hakuwa akitumia neno uchawi alisema watu wenye akili.
Neno hilo lilimaanisha uchawi, na wachungaji wengi wa kizungu hutumia sihili (uchawi) katika miujiza yao. Wakati wakimshangaa shangaa ofisini humo, yule mheshimiwa alichukua bastola yake na kuiweka mdomoni mwake, alifyatua na kusambaza ubongo wake nyuma ya kichwa kisha akadondoka chini.
Miguu yake akabaki akiirusharusha mfano wa mwanambuzi aliyechinjwa. Mtoto THE BOMBOM haraka aliwahi kuichukua bastola hiyo kisha akasogea kichwani mwa mheshimiwa huyo, damu zilikuwa zikitiririka mfano wa bomba la maji.
Alipofika maeneo ya kichwa kilipokuwa kimelala sakafuni, aliinama akatema mate akayachanganya na vumbi kisha akayapaka kichwani mwa mheshimiwa huyo. Baada ya dakika chache mheshimiwa huyo alisimama akiwa hai, wajumbe wa kikao hicho walijikuta wakishangilia miujiza hiyo iliyokuwa ikifanywa na mtoto huyo.
Hakukuwa na damu wala chembechembe ya ubongo ofisini humo, yule mheshimiwa akajikuta akiinama na kusujudu mbele ya mtoto THE BOMBOM.
Kila mmoja chumbani humo alijawa na nguvu za uponyaji, walibaki wakimuita mtoto huyo kuwa nabii. Badala ya kikao kukageuka kuwa eneo la sala, mapambio ya kila aina yalitamalaki ofisini humo.
Wanafunzi waliokuwa nje walishangaa kusikia miujiza hiyo, huo ndio ukawa mwanzo wa SURVIVE FROM THE DEATH CHURCH.
Mtoto THE BOMBOM aliwasihi sana wafuasi wake wa mwanzo kutotangaza miujiza ya namna hiyo, hakutaka kujitangaza mapema kwa kuwa alikuwa na sababu maalumu kichwani mwake. Aliwazuia kutangaza kashifa mbaya ya mheshimiwa yule, kisha akamsisitiza kuwa aachane na Padri huyo.
Kikao kilitamatika kila mmoja akiwa na imani kuu kwa mtoto huyo, miujiza aliyoiona mbele ya macho yake ilikuwa mikubwa sana. Kamati ya ulinzi na usalama waliondoka huku wakiahidi kufika eneo hilo mara kwa mara.
Ndugu msomaji jina la kanisa la kichawi limepatikana, unadhani nini kinafuata? Endelea kufuatilia kisa hiki cha kusisimua.
MHOLA?