NA WILLIAM BOMBOM
Ilipoishia...alipokodoa zaidi kuangalia eneo hilo alishangaa kuwaona majoka waliokuwa wamezunguka kambi hiyo huku wakitema moto uliokuwa ukiunguza kambi.
Endelea
Aliamua kupandisha ungo wake kwa juu akihofia kupata ajali ya kujitakia. Moto ulienea eneo zima la kambi ukiwaka kwa fujo, alipofika juu zaidi alichukua dawa fulani na kuinyunyiza eneo hilo.
Ghafla ule moto haukuonekana tena, hata wale majoka waliokuwa wakiusababisha hawakuonekana tena. Eneo lote la kambi lilikuwa shwari kabisa, akabaini moto huo ulikuwa ni zindiko la kambi.
Alishusha taratibu ungo wake na kutua eneo salama, pale chini aliwakuta wachawi wachache wakimsubiria. Waliongozana kuingia kwenye jengo walilokuwa wanafanyia kikao, mule ndani waliwakuta wachawi wengine wamefika. Kulikuwa na idadi kubwa ya wachawi ambao wengine walikuwa ni wageni machoni mwa mtoto THE BOMBOM.
Kulikuwa na wachawi wa rika zote, walikuwepo vijana ambao walikuwa wakijifunza taaluma hiyo, watu wa makamo na wazee. Ajenda kubwa zilizojadiliwa zilihusu njia bora za kuendeleza taaluma hiyo.
Walijadili kwa kina huku kila mmoja akitoa mchango wake, ukafika muda mtoto huyo akapewa nafasi ya kueleza. Ikumbukwe yeye alikuwa miongoni mwa viongozi kumi wa juu katika kambi hiyo, alikuwa bado hajaanza kufanya vimbwanga vyake.
Ndugu zangu ipo haja ya kubadili namna ya uendeshaji wa taaluma yetu. Uchawi ni taaluma kama zilivyo taaluma zingine, siyo mbaya kama tutawaiga watu weupe.
Alipofika hapo alitulia kidogo kuwapima makutano kama walikuwa wakimuelewa kisha akaendelea, "Dini zote tunazoziona duniani zilianzishwa na kundi dogo la watu, baadaye zikakua na kusambazwa duniani. Dini hizo huwa na malengo zaidi ya moja, watu wengi hutambua lengo moja tu ambalo ni kumtumikia Mungu".
Malengo yaliyo nyuma ya pazia hubaki kuwa siri, ni watu wachache sana ambao huelezwa malengo ya kweli. Ndugu zetu watu weupe wamezitumia ipasavyo kueneza tamaduni zao, wamehakikisha wanajifunza uchawi wa kwetu na kuupeleka makwao kupitia wapelelezi wa kwao. Hata sisi hatujachelewa tunaweza kutumia misingi hiyo, lakini tukaweka miko ya taaluma yetu.
Kwa mfano leo nimeamua kuanzisha kanisa linaitwa SURVIVE FROM THE DEATH, kanisa hili litasajiliwa kwa taratibu na sheria za nchi. Tutatengeneza katiba yetu ambayo itaonesha malengo ya uongo ili kurahisisha kupata vibali toka serikalini.
Kwa kuwa mpaka sasa waheshimiwa na wakuu wa idara zote halmashauri ni waamini wa kanisa hilo itatusaidia kupata vibali. Tutatumia bibilia kuhubiri yaliyomo, ila tutawaponya kwa nguvu za kichawi.
Alipofika hapo akatulia kidogo kupima kama alichokuwa akiongea kilieleweka, wachawi wengi walikuwa makini kumsikiliza mtoto huyo.
Alikuwa na uelewa wa hali ya juu, katika akili ya kawaida hakuna mchawi hata mmoja aliyewahi kufikiria kuanzisha taasisi ya kichawi imara kwa kufuata taratibu za serikali.
Mtoto huyo aliendelea, kwa kuwa malengo ya ndani ya taasisi hiyo ni kuendeleza uchawi ni lazima ujenzi wa kanisa hilo uzingatie sheria za kichawi. Lazima tumwage damu za binadamu wa kutosha kama ilivyo kawaida, nadhani hata ujenzi wa kambi hii imemwagika damu ya kutosha.
Katika kanisa hilo lazima kuwepo na zindiko kali, hii itatusaidia kuwazuia wenzetu kuingia watakavyo. Faida za kuanzisha kanisa hilo ni nyingi, tutaweza kupata wanachama wa kutosha wa uchawi.
Maana tutahakikisha kila tutakayemuhitaji kuwa mwanachama wetu wa kichawi atajiunga. Pili tutakuwa huru kwenda mahali popote kufanya kazi zete za kichawi kwa kisingizio cha kuhubiri. Tutakuwa na taasisi imara ambayo itatuingizia fedha za kutosha.
Katika kanisa hilo kila mmoja atakabidhiwa majukumu yake ya uficho, ili kufanikisha adhima yetu. Alihitimisha kwa kufafanua faida kedekede za kuanzishwa kwa kanisa hilo.
Kikao chote kwa pamoja walikubaliana mawazo hayo, walimshangaa mtoto huyo kwa kuwa na uelewa mkubwa kiasi hicho.
Walipanga mipango mingi ya namna ya kuweka misingi imara ya kanisa hilo, walimwaga madawa yao ili kujua eneo zuri la kujenga kanisa hilo. Hatimaye walikubaliana kuwa kanisa hilo lijengwe maeneo ya Isangejo, eneo hilo lipo barabarani hivyo kurahisisha kufikika kwake.
Pia eneo hilo lilikuwa mbali kidogo na kambi ya Ihushi, kwani isingependeza taasisi hizo zikawa karibu karibu. Maeneo hayo pia yalikuwa wazi, kupata hekari zaidi ya mia moja ingewawia rahisi.
Eneo hilo lilikusudiwa kuwepo kwa huduma pia za kijamii mfano hospitali, shule nk. Uwepo wa hospitali ungesaidia kupata vizimba vya aina mbalimbali vitakavyohitajika pasi kutumia nguvu. Uwepo wa wanafunzi kutasaifia kuwaendeleza katika taaluma ya kichawi ili baadaye wawe viongozi wa taasisi hiyo na serikali kwa ujumla.
Iliundwa kamati ndogo ya wachawi ishirini ya kuratibu shughuli nzima ya ujenzi wa kanisa hilo, mtoto THE BOMBOM alikuwa miongoni mwao.
Walipewa majukumu pia ya kuhakikisha linapatikana eneo lenye ukubwa wa kutosha, hilo halikuwa tatizo kwa upande wa kamati hiyo maana wangelitumia madawa kuyapata maeneo husika.
Hoja hiyo ilitamatika muda wa saa sita usiku, ikaingia hoja nyingine. Alisimama binti mdogo kisha akaanza kueleza shida yake, alielezea kuwa alibahatika kuingia kwenye mahusiano ya kimapenzi na kijana mmoja. Kijana huyo alikuwa ni mtoto wa katikista wa kigango cha Ihushi.
Katika mahusiano yao binti huyo alipewa ujauzito akiwa bado shule, walimu walipobaini hilo walimuitisha binti huyo kwa lengo la kumtaja aliyempa mimba. Binti huyo hakumtaja kwa makubaliano ya kuoana baadaye ili wamtunze mtoto wao.
Familia ilimlazimisha binti huyo kumtaja lakini hakutaja, mwalimu Mkuu wa shule hiyo alitumia kila hila, lakini hakufanikiwa. Binti huyo alipelekwa kituo cha polisi Kisesa ili akalazimishwe kumtaja muhusika, lakini hakumtaja.
Hatimaye akafukuzwa shule na kurudi makwao, alilea mimba yake mpaka akajifungua mtoto wa kiume. Mwanzoni mahusiano yao yalikuwa mazuri, mtoto huyo wa katikista alikuwa akumuhudumia binti huyo kwa kificho. Kiuchumi alikuwa vizuri kwa kuwa alikuwa akimiliki duka pale kijijini.
Baada ya binti huyo kujifungua kijana huyo alibadilika, alimtelekeza mtoto wa watu kisha akapata nesi mmoja aliyekuwa kituo cha afya cha Ihushi. Kijana yule aliota kiburi baada ya kuona binti huyo alishajifungua, mbaya zaidi hakutoa matumizi pia akawa ni mtu wa dharau.
Akatangaza kufunga ndoa na nesi huyo, kwa mjibu wa ratiba ndoa ilikuwa inafungwa siku ya kesho yake. Kwa hiyo binti alileta lalamiko hilo akitaka ndoa hiyo isitishwe, alionekana kumpenda mpenzi wake lakini kijana hakujishughulisha naye tena.
Hapa niseme kidogo, wanaume wengi mmekuwa mkiwadanganya watoto wa wenzenu kuwaoa, pindi unapopata ulichokuwa unakihitaji huwa tunawatelekeza.
Chondechonde kama hauna malengo ya kumuoa mtoto wa watu usimdanganye, mwambie tu nia yako maana kuna siku itakutokea puani. Basi kikao kilichukizwa sana na tabia ya kijana huyo, kwa pamoja wakakubaliana kwenda kumshikisha adabu.
Mambo mengine yaliendelea hadi muda wa saa saba, baada ya hapo waliteuliwa wachawi kumi kwenda kumshikisha adabu kijana huyo akiwemo na mtoto THE BOMBOM.
Wachawi hao waliambatana na yule binti aliyeleta malalamiko. Walichukua umbo la bundi kisha wakaruka kwa mbawa zao, walikwenda kutua karibu na mji wa kwao na kijana huyo.
Kulikuwa na watu wengi waliokuwa wakicheza disko vumbi, yote hayo yalikuwa ni maandalizi ya ndoa ya kesho yake. Lengo la wachawi hao ilikuwa ni kumuua kabisa kijana huyo, mikononi mwao walikuwa na misumari mitatu ya nchi sita na nyundo. Walidhamiria kumuua kikatili ili kukomesha tabia za wanaume za namna hii. Ndugu msomaji unadhani nini kitampata kijana huyo? Ungana nami katika simulizi hii ya kusisimua.
NANOGA.