NA WILLIAM BOMBOM
Ikafika zamu ya mchawi mwingine, safari hii mtoto THE BOMBOM aliwasogelea ili aweze kuchagua zamu ya mmoja wao. Wakati akiwasogelea...
Endelea
Wale wachawi walianza kurudi nyuma huku wakiwa hawaamini walichokuwa wakikiona mbele yao. Mtoto THE BOMBOM alipowakaribia alimchagua mwana mama mmoja aliyeonekana ni mtu wa makamo.

Licha ya mtoto THE BOMBOM kuwa na umbile dogo, lakini alifanikiwa kumvuta mchawi huyo hadi eneo lililokuwa likitumiwa kuondoa uhai wao chumbani humo.
Kabla hajafanya jambo lolote dhidi ya mchawi huyo, mtoto THE BOMBOM alinong'ona jambo na bibi yake kisha akaingia chumba kingine.
Punde si punde alirejea akiwa na kiboko mkononi, kilikuwa ni kiboko ambacho hutumiwa na wachawi kuwachapa watu.
Hapa niseme kidogo, ndugu msomaji naomba utambue kuwa wachawi hawatumii viboko vya kawaida kama wanavyotumia walimu mashuleni.
Viboko vya kichawi ni aina fulani ya nyasi zinazotumika kuezekea nyumba au mabafu na vyoo majumbani kwetu.
Siyo nyasi zote za aina hiyo hutumika bali zile ambazo hutoa maua ya kufanana na funza ni bora zaidi. Hizi nyasi nazo zipo za aina mbalimbali, hapa pia kuna kigezo ambacho hutumiwa zaidi kuzichagua.
Majani hayo hukaushwa kwa kutumia madawa kisha huchanganywa na madawa mengine ya kuongeza uchungu.
Hivi ndivyo huitwa viboko vya kichawi, viboko hivi hutofautiana kulingana na lengo la wachawi husika.
Mfano kama lengo la wachawi ni kumuua mtu kwa viboko, basi huwa kuna viboko vyenye nguvu ya kuua. Kama ndugu yako amekufa kifo cha ghafla, ukimpaka mafuta ya taa mwili mzima iwapo kifo hicho kimetokana na viboko vya kichawi utaona alama mwilini mwake.
Iwapo lengo la viboko hivyo ni kumchukua mtu huyo awe msukule, nyasi hizo huwekewa dawa ya uchungu.
Kuna watu hupotea kiajabu ajabu ndani ya jamii kumbe wako kwenye kambi za kichawi. Kabla ya kuchukuliwa huwa wanachapwa kiboko kimoja tu cha aina hii, kiboko hicho huwa na uchungu mara elfu ya uchungu wa kujifungua. Hata uwe mbishi kiasi gani ni lazima utafuata maelekezo ya wachawi waliokukamata.
Vipo viboko ambavyo hutumiwa kukata mizimu ya misukule wasumbufu. Wapo misukule ambao huwasumbua sana wachawi, hii hutokana na uimara wa mizimu ya mtu huyo au kosa lilifanyika katika taratibu za kumuchukua.
Ili kukata mizimu ya mtu huyo hurudishwa nyumbani kwao usiku wa manane. Akifikishwa nyumbani kwao huruhusiwa kuwaita ndugu zake kwa majina, mkiamka na kumsikia akiita majina yenu huanza kuchapwa na kurudishwa kambini.
Viboko ambavyo hutumiwa huwa na dawa ya namna hiyo, ni viboko vyenye uchungu mkubwa sana. Kama utasikia sauti ya ndugu yako usiku wa manane akiwa anawaita majina, kisha ukasikia sauti ya viboko anachapwa basi tambua wamemuleta kukata mizimu yake.
Basi baada ya mtoto THE BOMBOM kuleta kiboko hicho wale wachawi walibaini kilikuwa ni kiboko cha kuua.
Hii haikuwapa shida kulibaini hilo kwa kuwa na wao walikuwa ni wachawi kwa namna moja viboko vya namna hii walikuwa wakivitumia vyema.
Mtoto huyo alimsogelea mchawi huyo na kukinyanyua juu kiboko chake, yule mchawi alikuwa akilia mithili ya mtoto aliyelelewa malezi ya kizungu ya kudekezwa kipumbavu.
"Kwa nini mlitaka kuniteka?" Lilikuwa ni swali la kushitukiza toka kwa mtoto THE BOMBOM alilomuuliza mchawi huyo.
"Nisemehe sana, hayakuwa makusudi yetu bali yule Padri Samson Mcjohn alitulazimisha tukukamate. Yeye ndiye kiongozi wetu japo ni kiongozi pia wa kiroho parokia ya Masanza katika jimbo kuu la Magu. Yule mchawi alikuwa akiongea kwa uchungu, maumivu aliyokuwa ameyapata toka anakamatwa mpaka muda huo yalikuwa makali kupita maelezo. Wahenga walisema " mkuki kwa nguruwe..."
Kwa kuwa bibi alikuwa karibu na mchawi huyo alimnasa kibao kikali machoni mwake. Kisha akalishika sikio la mchawi huyo akaanza kulivuta kwa nguvu, mchawi huyo alipiga kelele kwa uchungu aliokuwa akiusikia lakini haikumsaidia.
Bibi aliliachia sikio hilo kisha akamtupia maswali mawili mfululizo "kwa nini mmeingia kwenye himaya yangu pasipo taarifa? Unadhani nikija na washirika wangu huko Masanza pasipo mawasiliano mtapenda?.
Yule mchawi alihema kidogo kushusha maumivu kisha kwa taabu aliamua kujibu. "Tusamehe mkuu, tuwie radhi kwa makosa tuliyoyafanya. Kamwe hatutarudia tena kufanya makosa haya" Baada ya hapo bibi alimuita mjukuu wake kisha walikaa pembeni kidogo wakajadili, yalikuwa ni majadiliano baina yao hivyo hakuna mtu mwingine aliyeelewa kilichozungumzwa.
Maongezi hayo yalipokamilika bibi aliingia chumbani, baada ya dakika kadhaa alikuja na dawa zilizokuwa zimehifadhiwa kwenye vyombo maalumu.
Alimkabidhi mtoto THE BOMBOM mikononi mwake, kisha mtoto huyo alizifungua dawa hizo na kuanza kuwapaka wachawi hao mateka.
Alipokamilisha shughuli hiyo, bibi aliwatemea mate huku akinuia maneno fulani. Punde si punde wachawi wale walitoweka maeneo hayo, kupitia nguvu ya madawa hayo walisafiri toka nyumbani kwa bibi hadi makwao.
Walipofika huko hawakuchukua muda mrefu wakafa, hii ilimtia wasiwasi Padri Samson Mcjohn kwa kuwa hakuelewa walichokuwa wamefanyiwa wafuasi wake.
Usiku ulipoingia Mtoto THE BOMBOM na bibi yake walielekea shereheni, siku hiyo kulikuwa na ugeni wa wachawi wa Bariadi walikuwa wamekuja kuwatembelea wachawi wa Magu.
Ilikuwa ni sherehe kubwa ambayo iliambatana na kubadilishana dawa na misukule. Wachawi walikula na kunywa, kulikuwa kumechinjwa ng'ombe wa kutosha.
Pia walichinjwa mbuzi na kondoo wasio na idadi kwa ajili ya wachawi wasio na hadhi. Kwa upande wa wageni maalumu wao walichinjiwa binadamu wanane kama heshima, siku zote wachawi hufurahi wanapopewa nyama ya binadamu kwa kuwa ni tamu kuliko nyama yeyote ile.
Sherehe zilifanyika vyema maeneo ya kiwanja cha shule ya msingi Gw'atelesha, shule hii tuliichagua kufanyia sherehe zetu kwa kuwa ipo nje kidogo mwa mji wa Magu. Maeneo ya shule hii ni mazuri katika kufanya sherehe kwa utulivu, pia namna ya kushuka kwa usafiri wa wachawi mbalimbali ingeturahisishia.
Sherehe hiyo iliambatana na kubadilishana misukule, zipo sababu mbalimbali ambazo hupelekea wachawi kubadilishana misukule. Mojawapo ya sababu hizo ni pamoja na: uzee wa msukule, nguvu za msukule, usumbufu wake, vizimba nk.
Ndugu msomaji unadhani nini kitatokea kwenye sherehe hiyo ya kichawi? Je, mtoto THE BOMBOM atafanya tukio gani maeneo hayo? Ungana nami katika sehemu inayofuata.