Tanzania, Japan zasaini mikataba mitatu ya mkopo wenye masharti nafuu na msaada

NA BENNY MWAIPAJA-WFM

JAMHURI ya Muungano wa Tanzania na Japan kupitia Shirika lake la Ushirikiano wa Kimataifa (JICA), zimesaini mikataba mitatu ya mkopo wenye masharti nafuu na msaada, yenye thamani ya Yen bilioni 10.15, sawa na shilingi za Tanzania, bilioni 174.9, kwa ajili ya utekelezaji wa Mradi wa Ununuzi wa pemebejeo za kilimo pamoja na kufufua Shirika la Uvuvi Tanzania (TAFICO). 
Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango Dkt. Natu El-Maamry Mwamba na Balozi wa Japani nchini Tanzania Bw. Yasushi Misawa wakisaini hati ya mikataba ya mikopo yenye masharti nafuu na msaada yenye jumla ya Yen bilioni 10.15 sawa na shilingi bilioni 174.2 kwa ajili ya kuendeleza kilimo na uvuvi kupitia Wizara ya Kilimo na Wizara ya Mifugo na Uvuvi kwa kufufua Shirika la Uvuvi Tanzania (TAFICO), ambapo kupitia mradi huo TAFICO watarajia kununua meli ya kisasa ya uvuvi na miundombinu ya kuhifadhi samaki, huku sekta ya kilimo, mkopo huo utatumika kununua pembejeo za kilimo kama vile mbolea kwa ajili ya wakulima wadogo, utoaji wa mbegu bora na kuongeza uzalishaji wa mazao ya mpunga, ngano na alizeti.

Akizungumza baada ya kusaini mikataba hiyo kwa niaba ya Serikali, Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango, Dkt Natu Mwamba, alisema kuwa Yen bilioni 10 sawa na shilingi za Tanzania bilioni 172.2 ni mkopo nafuu uliotolewa na Shirika la Ushirikiano la Kimataifa (JICA) kwa kushirikiana na Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) na kiasi cha Yen milioni 150, sawa na zaidi ya shilingi za Tanzania bilioni 2.6, ni msaada uliotolewa na nchi hiyo kupitia Ubalozi wake hapa nchini. 
Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango Dkt. Natu El-Maamry Mwamba na Balozi wa Japani nchini Tanzania Bw. Yasushi Misawa wakibadilishana hati ya mikataba ya mikopo yenye masharti nafuu na msaada yenye jumla ya Yen bilioni 10.15 sawa na shilingi bilioni 174.2 kwa ajili ya kuendeleza kilimo na uvuvi kupitia Wizara ya Kilimo na Wizara ya Mifugo na Uvuvi kwa kufufua Shirika la Uvuvi Tanzania (TAFICO), ambapo kupitia mradi huo TAFICO watarajia kununua meli ya kisasa ya uvuvi na miundombinu ya kuhifadhi samaki, huku sekta ya kilimo, mkopo huo utatumika kununua pembejeo za kilimo kama vile mbolea kwa ajili ya wakulima wadogo, utoaji wa mbegu bora na kuongeza uzalishaji wa mazao ya mpunga, ngano na alizeti.

Dkt. Mwamba, alisema kuwa mkopo huo utatumika kuongeza tija katika kilimo kwa kununua pembejeo ikiwemo mbolea, mbegu bora kwa ajili ya wakulima ili kuongeza uzalishaji wa mazao ya kipaumbele ambayo ni mpunga, ngano na alizeti na kuweka mifumo bora ya upatikanaji wa chakula na lishe. 

Aliitaja mikoa itakayonufaika na mradi huo wa kuendeleza kilimo kuwa ni Arusha, Manyara, Kilimanjaro, Dodoma, Singida, Morogoro, Tabora, Songwe, Mbeya, Njombe, Shinyanga, Mwanza, Geita, Simiyu na Katavi. 
Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango Dkt. Natu El-Maamry Mwamba na Balozi wa Japani nchini Tanzania Bw. Yasushi Misawa wakionesha moja ya mikataba ya mikopo yenye masharti nafuu na msaada yenye jumla ya Yen bilioni 10.15 sawa na shilingi bilioni 174.2 kwa ajili ya kuendeleza kilimo na uvuvi kupitia Wizara ya Kilimo na Wizara ya Mifugo na Uvuvi kwa kufufua Shirika la Uvuvi Tanzania (TAFICO), ambapo kupitia mradi huo TAFICO watarajia kununua meli ya kisasa ya uvuvi na miundombinu ya kuhifadhi samaki, huku sekta ya kilimo, mkopo huo utatumika kununua pembejeo za kilimo kama vile mbolea kwa ajili ya wakulima wadogo, utoaji wa mbegu bora na kuongeza uzalishaji wa mazao ya mpunga, ngano na alizeti.

Kuhusu mradi wa kuendeleza sekta ya Uvuvi, Dkt. Mwamba alisema kuwa shilingi bilioni 2.6 zilizotolewa na Japan kama msaada, zitatumika kufufua Shirika la Uvuvi Tanzania (TAFICO), ikiwa ni nyongeza ya fedha za msaada wa Yeni milioni 200 sawa na shilingi bilioni 3.5 zilizotolewa na nchi hiyo kupitia mkataba uliosainiwa mwezi Disemba mwaka 2019 na hivyo kuufaya kufikia shilingi bilioni 6.2, lakini utekelezaji wake ulikwama baada ya kuzuka kwa UVIKO 19. 

Kwa upande wao, Balozi wa Japan Nchini Tanzania, Mheshimiwa Yashushi Misawa na Mwakilishi Mkazi wa (JICA), Bw. Hitoshi Ara, walisema kuwa mkopo na msaada huo umelenga kukabiliana na uhaba wa chakula unaoikabili dunia hivi sasa kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo uharibifu wa mazingira, vita vya Urusi na Ukraine pamoja na UVIKO 19. 
Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango Dkt. Natu El-Maamry Mwamba na Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Ushirikiano la kimataifa (JICA) Bw. Hitoshi Ara wakionesha hati ya mkataba ya mkopo yenye masharti nafuu ya Yen milioni 150 sawa na shilingi bilioni 2.6 kwa ajili ya kufufua Shirika la Uvuvi Tanzania (TAFICO), kwa kununua meli ya kisasa ya uvuvi na miundombinu ya kuhifadhi samaki.

Walisema kuwa Vitu hivyo vimeleta changamoto kubwa kwa sekta ya kilimo na usalama wa chakula kwa jumuiya ya kimataifa huku Afrika ikitajwa kuwa bara lililoathiriwa zaidi, na kuupongeza uongozi madhubuti wa Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuhakikisha Tanzania inajitosheleza kwa chakula na kufikia malengo yake ya kuifanya Tanzania kuwa ghala la chakula barani Afrika.

“Japan imekuwa ikiisaidia Tanzania kupitia JICA kwa zaidi ya miaka 60, ikihusisha maeneo mbalimbali ikiwa ni pamoja na maendeleo ya kilimo na uvuvi. Na kila mara tunajikumbusha kuwa maendeleo ya rasilimali watu yanapaswa kuwa nguzo muhimu katika aina yoyote ya usaidizi wa maendeleo,”amesema Balozi wa Japan nchini Tanzania,Mhe.Yashushi Misawa. 
Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango Dkt. Natu El-Maamry Mwamba (watatu kushoto), Balozi wa Japani nchini Tanzania Bw. Yasushi Misawa (watatu kulia), Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango Bi. Amina Khamis Shaaban (wakwanza kulia), Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi Prof. Riziki Shemdoe (wa pili kushoto) na Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Ushirikiano la Japan Bw. Hitoshi ARA wakiwa katika picha ya Pamoja nna ujumbe wa Tanzania na Japan baada ya hafla fupi ya kusaini mikataba ya mikopo yenye masharti nafuu na msaada yenye jumla ya Yen bilioni 10.15 sawa na shilingi bilioni 174.2 kwa ajili ya kuendeleza kilimo na uvuvi kupitia Wizara ya Kilimo na Wizara ya Mifugo na Uvuvi kwa kufufua Shirika la Uvuvi Tanzania (TAFICO), ambapo kupitia mradi huo TAFICO watarajia kununua meli ya kisasa ya uvuvi na miundombinu ya kuhifadhi samaki, huku sekta ya kilimo, mkopo huo utatumika kununua pembejeo za kilimo kama vile mbolea kwa ajili ya wakulima wadogo, utoaji wa mbegu bora na kuongeza uzalishaji wa mazao ya mpunga, ngano na alizeti.(Picha na WFM).

Kwa upande wake Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Profesa Riziki Shemdoe, alisema kuwa fedha za msaada kutoka Japan, zitatumika kununua meli kubwa ya uvuvi katika Bahari Kuu ya Hindi, kujenga miundombinu ya kuhifadhi samaki pamoja na vitendea kazi vingine vitakavyo tumika kuinua sekta ya uvuvi na kuiingizia Serikali fedha za kigeni. 

Alisema kuwa mradi huo ambao utatekelezwa kwa kipndi cha mwaka mmoja utakapo kamilika, pamoja na mambo mengine, unatarajia kuongeza ajira 20,000, na kuiingizia Serikali zaidi ya shilingi bilioni 200 kwa mwaka hivyo kuongeza mchango wake katika Pato la Taifa kwa kiasi kikubwa ikilinganishwa na mchango wa sasa wa asilimia 1.7. 

Naye, Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo, Dkt Hussein Omar aliishukuru Japan kupitia JICA kwa kuwekeza kiasi hicho cha fedha katika sekta ya kilimo ambayo imeajiri idadi kubwa ya watu. 

Alisema kuwa fedha hizo zitasaidia kuboresha kilimo kwa kuwawekea wakulima mazingira bora ya uzalishaji ikiwemo kuwapatia wakulima wadogo mbolea, mbegu bora, viuatilifu na huduma nyingine za ugani ili waweze kuzalisha mazao kwa wingi.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news