NA GODFREY NNKO
WAZIRI wa Afya, Mheshimiwa Ummy Mwalimu amesema kuwa, ushirikiano wa pamoja baina ya wananchi, wadau mbalimbali na Serikali umefanikisha kuudhibiti ugonjwa wa Marburg ulioripotiwa kuzuka mkoani Kagera hivi karibuni.
Mheshimiwa Ummy ameyasema hayo leo Aprili 29, 2023 jijini Dar es Salaam wakati akitoa taarifa ya mwenendo wa ugonjwa wa Marburg mkoani Kagera.
"Awali ya yote nimshukuru Mungu mwingi wa rehema kwa kuendelea kutujalia uhai na afya njema. Kama mnakumbuka tarehe 21 Machi 2023 tulitoa taarifa kwa umma juu ya uwepo wa watu wenye ugonjwa wa Marburg mkoani Kagera.
"Nafurahi kuwajulisha kuwa kuanzia tarehe 21 Aprili 2023 hatuna mgonjwa yeyote mwenye virusi vya ugonjwa huu mkoani Kagera hapa nchini.
"Wagonjwa wawili waliokuwa wamesalia katika vituo maalum vya matibabu waliruhusiwa kutoka tarehe 20 na tarehe 21 Aprili 2023 baada ya kuthibitika kimaabara kuwa hawana tena virusi vya Marburg,"amefafanua Mheshimiwa waziri Ummy.
Pia amesema,tokea tarehe 4 Aprili 2023, "nilipotoa taarifa yangu ya mwisho kwa umma kuhusu mwenendo wa ugonjwa huu, tulipata ongezeko la mgonjwa mpya mmoja ambaye ni mama wa mtoto wa umri wa miezi 18 aliyekuwa ametengwa na baadaye kuthibitika kuwa na maambukizi ya virusi vya Marburg.
"Hii inaonyesha kuwa hatua za haraka zilizochukuliwa na Serikali zilipelekea kuhakikisha ugonjwa huu hausambai nje ya familia zilizoathirika na kwa watumishi wa afya waliowahudumia wagonjwa kabla ya kuthibitika uwepo wa ugonjwa huu.
"Kwa ujumla, toka tulipotangaza uwepo wa ugonjwa huu mkoani Kagera tarehe 21 Machi 2023 hadi sasa, jumla ya watu waliopata maambukizi ni tisa, kati ya hao watatu wamepona akiwemo daktari aliyewahudumia wagonjwa wa mwanzo kabla ya kuthibitika.
"Aidha, wagonjwa sita walipoteza maisha akiwemo mtumishi mmoja wa afya mmoja na mtoto wetu mwenye umri wa miezi 18.
"Vilevile, ninafurahi kuwajulisha kuwa watu 211 kati watu 212 waliokuwa wametangamana na wagonjwa na kuwekwa karantini wameruhusiwa baada ya kumaliza siku 21 za ufuatiliaji bila kuonesha dalili za ugonjwa huu. Hii ni ishara kuwa jitihada za pamoja zilizofanyika katika kukabiliana na mlipuko huu zimeleta mafanikio makubwa,"ameongeza Mheshimiwa Waziri Ummy.
Amebainisha kuwa, kwa mujibu wa Mwongozo wa Shirika la Afya Duniani (WHO) kuhusu ufuatiliaji wa magonjwa ya mlipuko ikiwemo Ugonjwa wa Marburg, Serikali itaendelea na ufuatiliaji wa ugonjwa huu mkoani Kagera.
"Na endapo hakutatokea mgonjwa mpya mwenye virusi vya Marburg baada ya siku 42 tokea mgonjwa wa mwisho kuthibitika kutokuwa na maambuzi yaani ifikapo tarehe 31 Mei 2023 ndipo tutatangaza rasmi kumalizika kwa ugonjwa wa Marburg mkoani Kagera na nchini Tanzania kwa ujumla.
"Niwaombe wananchi kuendelea kuchukua tahadhari za kinga dhidi ya ugonjwa huu na magonjwa mengine ya kuambukiza. na kuendelea kutoa ushirikiano kwa wataalam wa afya kadri itakavyokuwa inahitajika.
"Serikali inaendelea kutoa shukrani za pekee kwa wataalam wa afya hususani walioko mstari wa mbele mkoani Kagera wakiwemo waliotoa huduma kwa wagonjwa (case management team), waliofanya ufuatiliaji wa watu waliotangaana na wagonjwa (contract tracing team), waliofanya vipimo,
"Walioshiriki katika maziko salama na ya heshima kwa waliofariki kwa ugonjwa wagonjwa (dignified burial team) na waliotoa Elimu kwa wananchi katika kipindi chöte tokea tulipotangaza uwepo wa mlipuko wa ugonjwa huu.
"Nitumie fursa hii kusisitiza umuhimu wa watumishi wa afya kuzingatia Kanuni na Miongozo ya Kuzuia na Kudhibiti Maambukiz kutoka wa wagonjwa (Infection Prevention and Control - IPC). Narudia tena kusisitiza watumishi kuzingatia Kanuni za IPC wakati wote wa kuhudumia wagonjwa.
"Kwa heshima na unyenyekevu mkubwa ninamshukuru Mheshimiwa Dkt.Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kutuwezesha kukabiliana na ugonjwa huu.
"Aidha ninamshukuru Mhe.Kassim Majaliwa (Mb.), Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kutuongoza vyema katika mapambano haya.
"Vilevile niwashukuru viongozi wote wa Mkoa wa Kagera, wananchi, wanahabari na wadau mbalimbali walioshirikiana nasi kwa hali na mali hadi sasa katika kukabiliana na ugonjwa huu nchini. Kipekee ninawashukuru Shirika la Afya Duniani (WHO), Shirika la Kuhudumia Watoto Duniani (UNICEF), Kituo cha Wamarekani cha Kuzuia na Kudhibitti Magonjwa ya Kuambikiza (US CDC), Madaktari wasio na Mipaka (MSF), Africa CDC na wadau wote wa ndani na nje ya nchi,"amefafanua Mheshimiwa Waziri Ummy Mwalimu.