NA MWANDISHI WETU
JAMHURI ya Muungano wa Tanzania na Jamhuri ya Malawi zimekubaliana kukuza uhusiano wa kibiashara na uwekezaji kwa kuboresha mazingira ya ufanyaji biashara na uwekezaji baina ya nchi hizo ikiwemo uboreshaji wa sheria za uwekezaji, ukamilishaji wa ujenzi wa Kituo cha Pamoja cha Kasumulo na huduma za Bandari ya Mbamba Bay ili kukuza biashara na uchumi katika nchi hizo.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Uwekezaji, Viwanda na Biashara, Dkt. Hashil Abdallah (katikati) kwa niaba ya Waziri wa Wizara hiyo, Dkt. Ashatu Kijaji akiwa na Waziri wa Biashara na Viwanda wa Malawi, Mhe. Simplex Chithyola Banda (Mb.) (wa pili kushoto) wakikagua mashine ya kukamulia maziwa kutoka Tanzania katika maonyesho ya bidhaa wakati wa Kongamano la Biashara na Uwekezaji kati ya Tanzania na Malawi linalofanyika Aprili 26 hadi 29,2023 Mzuzu nchini Malawi.
Hayo yamesemwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Uwekezaji, Viwanda na Biashara, Dkt.Hashil Abdallah tarehe 26 Aprili, 2023 kwa niaba ya Waziri wa Wizara hiyo, Dkt. Ashatu Kijaji alipokuwa akihutubia Kongamano la Biashara na Uwekezaji kati ya Tanzania na Malawi linalofanyika Aprili 26 hadi 29,2023 Mzuzu nchini Malawi.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Uwekezaji, Viwanda na Biashara, Dkt.Hashil Abdallah (kulia) kwa niaba ya Waziri wa Wizara hiyo, Dkt. Ashatu Kijaji akiongea na Waziri wa Biashara na Viwanda wa Malawi, Mhe. Simplex Chithyola Banda (Mb.) (kushoto) wakati wa Kongamano la Biashara na Uwekezaji kati ya Tanzania na Malawi linalofanyika Aprili 26 hadi 29,2023 Mzuzu nchini Malawi.
Aidha, amesema Tanzania inawakaribisha wawekezaji na wafanyabiashara kutoka Malawi kuja kuwekeza na kufanya biashara Tanzania katika sekta za kilimo, uvuvi, uchumi wa buluu, uzalishaji utalii, huduma za fedha, uchukuzi, miundombinu, mawasiliano, madini elimu na afya ili kukuza biashara na uchumi wa nchi hizo
Vilevile amewataka wafanyabishara na wawekezaji wa Tanzania kutumia kikamilifu fursa zinazopatikana baina ya nchi hizo kulingana na raslimali zilizopo katika nchi hizo ili kuongeza kasi ya ukuaji wa biashara ambayo imefikia kiasi cha dola za Marekani milioni 86.7 mwaka 2022.
Waziri wa Biashara na Viwanda wa Malawi, Mhe.Simplex Chithyola Banda (Mb.) (kulia) akifungua Kongamano la Biashara na Uwekezaji kati ya Tanzania na Malawi linalofanyika Aprili 26 hadi 29,2023 Mzuzu nchini Malawi.
Naye Waziri wa Biashara na Viwanda wa Malawi, Mhe.Simplex Chithyola Banda (Mb.) amesema Malawi iko tayari kuimarisha uhusiano wa kibiashara na uwekezaji baina ya nchi hizo uliopo tangu Uongozi wa Serikali ya Awamu ya Kwanza ya Tanzania kwa kuendelea kuboresha mazingira ya biashara nchini humo.
Wafanyabiashara wa Tanzania wakishiriki Kongamano la Biashara na Uwekezaji kati ya Tanzania na Malawi linalofanyika Aprili 26 hadi 29,2023 Mzuzu nchini Malawi.
Aidha, amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe.Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa msaada wa chakula na vifaa vya kujihifadhi alioutoa wakati Malawi ilipokumbwa na kimbunga Freddy mwezi Machi 2023.
Aliyekuwa Balozi wa Tanzania nchini Malawi, Mhe. Humphrey Polepole ( kushoto) akiongea na Waziri wa Biashara na Viwanda wa Malawi, Mhe.Simplex Chithyola Banda (Mb.) (kulia) wakati wa Kongamano la Biashara na Uwekezaji kati ya Tanzania na Malawi linalofanyika Aprili 26 hadi 29, 2023 Mzuzu nchini Malawi.
Kwa upande wa wake aliyekuwa Balozi wa Tanzania nchini Malawi, Mhe. Humphrey Polepole amesema kongamano hilo limewakutanisha wafanyabiashara na wawekezaji zaidi ya 300 kujadili, na kutatua changamoto mbalimbali zinazowakabili katika biashara zao baina ya nchi hizo.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Uwekezaji, Viwanda na Biashara, Dkt. Hashil Abdallah (kushoto) akiwa na aliyekuwa Balozi wa Tanzania nchini Malawi, Mhe. Humphrey Polepole (wapili kushoto) wakishiriki.
Picha ya pamoja ya viomgozi wa Tanzania na Malawi walioshiriki Kongamano la Biashara na Uwekezaji kati ya Tanzania na Malawi linalofanyika Aprili 26 hadi 29,2023 Mzuzu nchini Malawi.
Pia amewashauri watanzania kuwa wabunifu na kushirikiana na wafanyabiashara wa Malawi kutumia fursa za biashara na uwekezaji zilizopo nchini Malawi ambayo ni moja ya nchi sisizokuwa na bahari.