NA MWANDISHI WETU
ALIYEWAHI kuwa Mbunge wa Musoma Vijijini na Butiama mkoani Mara, Nimrod Mkono amefariki dunia akiwa nchini Marekani alikokuwa akitibiwa tangu mwaka 2018.
Akizungumza kwa simu na Gazeti la Mwananchi leo Aprili 18, mdogo wa marehemu, Zadock Mkono amethibitisha kutokea kwa kifo hicho akisema kimetokea Florida nchini Marekani.
“Taarifa ni za kweli, hata mimi nimezungumza na binti yake na mkewe wamesema kuwa amefariki leo aubuhi huko Amerika. Alikuwa anatibiwa nchini Marekani katika jimbo la Florida miaka minne iliyopita na sasa unaingia mwaka wa tano,”amesema.
Amesema, Mkono alikuwa akisumbuliwa na ugonjwa wa kupoteza kumbukumbu.“Nimeongea na ndugu kule wanasema mwili utaletwa kuzikwa Tanzania, japo utachelewa,”amesema.
Mkono, aliyezaliwa Agosti 18, 1948, Busegwe mkoani Mara alikuwa mwanasheria na mwanasiasa maarufu.Pia ni Ni mwanzilishi wa kampuni ya mawakili ya Mkono & Co, yenye makao makuu yake jijini Dar es Salaam.(Mwananchi)