APRILI 5, 2023 Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Kassim Majaliwa bungeni jijini Dodoma amewasilisha hotuba kuhusu Mapitio na Mwelekeo wa Kazi za Serikali na Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Ofisi ya Waziri Mkuu na Ofisi ya Bunge kwa mwaka 2023/2024.Tazama hapa chini hotuba yote;
"Mheshimiwa Spika, kwa mwaka 2023/2024, Ofisi ya Waziri Mkuu na taasisi zilizo chini yake inaliomba Bunge lako tukufu liidhinishe jumla ya shilingi 173,733,110,000. Kati ya fedha hizo, shilingi 121,364,753,320 ni kwa ajili ya matumizi ya kawaida na shilingi 52,368,356,680 ni kwa ajili ya matumizi ya maendeleo.
"Mheshimiwa Spika, vilevile naliomba Bunge lako tukufu liidhinishe jumla ya shilingi 165,627,897,000 kwa ajili ya Mfuko wa Bunge. Kati ya fedha hizo, shilingi 160,458,877,000 ni kwa ajili ya matumizi ya kawaida na shilingi 5,169,020,000 ni kwa ajili ya matumizi ya maendeleo,"amehitimisha Waziri Mkuu.