Tunatarajia ushindi mkubwa-Waziri Dkt.Chana

NA MWANDISHI WETU

WAZIRI wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Balozi Dkt. Pindi Chana amekabidhi Bendera ya Taifa kwa Timu ya Fountain Gate inayokwenda nchini Afrika Kusini kwenye Mashindano ya Soka la Wanawake Afrika kwa Shule za Sekondari yanayotarajiwa kufanyika mwezi huu wa Aprili, 2023.
Tukio hilo limefanyika jijini Dar es Salaam, ambapo amewasihi wachezaji hao watambue ukubwa wa mashindano hayo kwa kuwa hawaiwakilishi Tanzania pekee bali Ukanda wa Afrika Mashariki na Kati.

"Mtakapokuwa nchini Afrika Kusini, hakikisheni mnapeperusha vyema Bendera yetu, mkafanye vizuri lakini pia mzingatie maadili, mila na desturi za nchi yetu pamoja na kutangaza lugha ya Kiswahili,"amesema.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Fountain Gate, Bw. Japhet Makau amesema, shule hiyo imeendelea kufanya vizuri katika michezo ambapo ina wachezaji katika Timu ya Taifa ya Wanawake, pamoja na timu inayoshiriki na kufanya vizuri katika Ligi kuu ya Wanawake nchini.

Timu hiyo ya Fountain Gate ndiyo wawakilishi wa ukanda wa Afrika Mashariki na Kati CECAFA huku ukanda mwingine ni UNAF ambao ni Afrika Kaskazini,WAFU wa Afrika Magharibi na UNIFFAC wa Afrika ya Kati.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news