Tuwaheshimu wanaojitoa sadaka kwetu-Padri Thomas Akito

NA ADELADIUS MAKWEGA

WAKRISTO wametakiwa kutambua kuwa katika ulimwengu wa leo wapo watu mbalimbali wanaojitoa sadaka kwa ajili ya wengine katika kila siku inayokwenda kwa Mungu ndiyo maana Mtume Petro analisitiza hilo. 
Hayo yamesemwa na Padri Thomas Akito katika misa ya Jumapili ya tatu baada ya Pasaka ya Aprili 23, 2023 katika Kanisa dogo ndani ya makazi ya watawa wa Rosimini kando ya nyumba ya malezi ya Masista Wakarmeli wa Mtakatifu Teresia wa Mtoto Yesu Lushoto Mjini, Jimbo Katoliki la Tanga. 

“Je, jamii yetu inatambua hilo? Je chakula kikifika mezani kimefika bure? Watoto mpo? Ili chakula kifike mezani kimefika bure? Ili utupie mpunga unakuja bure? Si kuna mtu amenunua na kukitengeneza?.

"Haujaja bure jamani, tuwatambue wale wanaojitoa sadaka kwa ajili yetu kila siku. Wengine vingine tunaviona vitu vipo tu, lakini hatujiuliza je vimetoka wapi. Nawaombeni kuanzia sasa tujiulize hilo.” 
Akiendelea kuhubiri katika misa hiyo katika kanisa dogo linaloweza kujaza waamini 60 lililopambwa kwa picha za Mtakatifu Bakita, kukiwa na watawa 34 na familia moja yenye watu watano, Padri Akito alisema kuwa,

“Ni vizuri sana kushukuru watu wanaotumia walichonacho kuwasaidia wengine, Yesu kabla ya kutukomboa alifika na kuwa nasi jirani na kuyaishi maisha ya mwanadamu, hapo alitoa nafasi ya kutukaribia kama alivyowafuata hawa mitume wawili njiani. 
"Sasa ni wakati wa kila mmoja wetu kuwashukuru mno wazazi, walezi na walimu wetu ambao wametulea.Tusiyatazame madhaifu yao tu, hata kama walituadhibu hiyo ilikuwa na hatua mojawapo ya malezi, vinginevyo bila wao tusingeonekana kama hivi tulivyo leo hii.” 

Misa hiyo iliyosindikizwa na nyimbo zilizoimbwa na kwaya ya watawa wa Karmeli iliambatana na nia kadhaa za misa kutoka kwa watawa wa hao na maombi kadhaa ya dominika hii na mojawapo lilikuwa hili, 
“Utuondolee, hofu, wasiwasi na mashaka yote katika kukufuata wewe.” Wakati misa hiyo inafanyika hali ya hewa ya eneo la Lushoto mkoani Tanga kwa juma zima ni baridi,mawingu, ukungu na mvua kubwa zilizofululiza kunyesha, huku wakulima wakipalilia viazi, maharage na mazao mengine ya bustani milimani.

Japokuwa kunyesha kwa mvua kubwa kwa baadhi ya wakulima wale wanaolima katika vitivo sasa kilimo biashara cha bustani katika vitivo bondeni hakifanyiki maana vitivo vyote vimejaa maji, nafuu inatarajiwa mara baada ya mvua kubwa kumaliza ndipo kilimo katika vitivo vyote vya mabondeni vitaendelea. 

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news