NA LWAGA MWAMBANDE
REJEA katika Biblia Takatifu kitabu cha 1 Wakorintho 14:33... "Kwa maana Mungu si Mungu wa machafuko, bali wa amani; vile vile kama ilivyo katika makanisa yote ya watakatifu."
Aprili 24, 2014 Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa katika makao makuu ya Umoja wa Mataifa huko jijini New York, Marekani lilifanya mjadala wa siku mbili kuhusu umuhimu wa jamii tulivu na zenye amani katika kufanikisha utekelezaji wa Malengo Endelevu ya Maendeleo ya Umoja wa Mataifa ya 2030, baada ya mwaka 2015.
Kupitia mjadala huo, aliyekuwa Rais wa Baraza Kuu, John Ashe katika hotuba yake alifafanua kuwa, utulivu na amani ni muhimu katika kuwezesha maendeleo endelevu, ikiwa ghasia kwa maana ya vita vitapata nafasi, hiyo itakuwa ni moja ya vikwazo vikubwa vya maendeleo hayo.
Ashe wakati huo alisema, ni jambo la kutia moyo kuwa vita na migogoro kati ya nchi na nchi vimepungua, lakini bado utulivu na ghasia ndani ya nchi vimeongezeka na kusababisha vifo na machungu kwa raia.
1.Uko kwenye mapambano, hili la kujiuliza,
Wala si la mkutano, na watu kuwaagiza,
Ujitafakari mno, fikira zote kumeza,
Vita vyapiganwa wapi?
2.Jibu utalolipata, laweza kukueleza,
Kuiendeleza vita, na mbele kujipongeza,
Au suluhu kupata, usizidi jiumiza,
Vita vyapiganwa wapi?
3.Kama vyapiganwa kwako, huko unakojilaza,
Wafao ni watu wako, na wengi wawauguza,
Kunaisha huko kwako, zidisha kujiuliza,
Vita vyapiganwa wapi?
4.Ukisema umeshinda, huyo memgaragaza?
Au mwendo unakwenda, kwako anakulegeza?
Nyoka bila ya kupinda, shida utaimaliza,
Vita vyapiganwa wapi?
5.Ona vyapiganwa kwako, ndiwe anakuburuza,
Huko kuinuka kwako, yeye anakutuliza,
Wala hunacho kicheko, jinsi anakuumiza,
Vita vyapiganwa wapi?
6.Umaskini jeuri, unaweza jimaliza,
Hata uwe ni jasiri, nguvu anakulegeza,
Marafiki matajiri, damu yao waitunza,
Vita vyapiganwa wapi?
7.Heri pata nusu shari, kuliko kukumaliza,
Akuzidi uhodari, huwezi ukamuweza,
Kwa maneno we fahari, vitendo agaragaza,
Vita vyapiganwa wapi?
8.Historia twasoma, wale waliojiweza,
Vita kama amepima, hawezi akaiweza,
Kwa maneno alisema, pita na kupitiliza,
Vita vyapiganwa wapi?
9.Damu nyingi yamwagika, wewe unajipongeza,
Miundombinu yalika, wageni wakupongeza,
Ndiyo unamalizika, kuinuka hutaweza,
Vita vyapiganwa wapi?
10.Jinsi muda unapita, ubishi kupitiliza,
Misaada nayopata, akili yakupumbaza,
Mwisho wake utakuta, amekwisha kumaliza,
Vita yapiganwa wapi?
11.Kama ningekuwa mimi, tembo anajitukuza,
Ngekuwa mpole mimi, asije nigaragaza,
Uzito wake sisomi, kwake najiegemeza,
Vita vyapiganwa wapi?
12.Pia ninyi marafiki, mwampongezapongeza,
Misaada kinafiki, mwajua ajimaliza,
Ni sawa na mamluki, apigwe mnateleza,
Vita vyapiganwa wapi?
13.Tunateseka dunia, vita kuviendeleza,
Bei zinatuzidia, hamtaki kumaliza,
Yatikisika dunia, kesho ngumu kuiwaza,
Vita vyapiganwa wapi?
Lwaga Mwambande (KiMPAB)
lwagha@gmail.com 0767223602

Pia, alisema hali hiyo ikiendelea suala la kutokomeza umaskini litabakia ndoto kwa wengi iwapo jamii ya kimataifa haitashirikiana kumaliza migogoro, ukosefu wa utulivu, kuongeza ujumuishi, uongozi bora na maendeleo kwa wote.
“Kufikia lengo kuu la kutokomeza umaskini kutabakia ndoto kwa wengi iwapo hatutashirikiana kumaliza migogoro na ukosefu wa utulivu, halikadhalika kuongeza ujumuishi, uongozi bora, utawala wa kisheria, haki za binadamu na haki ya maendeleo kwa wote.”
Aidha, licha ya juhudi mbalimbali zinazoendelea katika ngazi za kitaifa na Kimataifa, Dunia imeendelea kushuhudia mikinzano ya mara kwa mara ambayo imechangia mambo mengi kuendelea kudorora ikiwemo uchumi, kupoteza nguvu kazi na hata kusambaratisha mipango ya kijamii.
Mshairi wa kisasa, Lwaga Mwambande licha ya kuhoji vita vyapiganwa wapi? Bado anaendelea kusisitiza kuwa, ikiwa jamii ni jambo la lazima kwa mwanadamu ambalo haepukani nalo, na ndio inayojenga mustakabali na hadhi ya mwanadamu kuanzia kwake binafsi na mbele ya jamii nyingine basi ni lazima jamii hiyo itunzwe na ienziwe ili idumu katika uasili wake ambao ni amani, utulivu na umoja kama vinavyoelekeza vitabu vitakatifu vya Mungu. Endelea;.