NA MWANDISHI WETU
FAINALI ya Michuano ya Kombe la Masauni na Jazeera Cup imefikia tamati ambapo yameibua Timu ya Mnazi Mmoja kuchukua zawadi ya Kitita cha Shilingi Milioni Mbili (2,000,000) pamoja na zawadi mbalimbali ikiwemo jezi na kiatu cha dhahabu cha mfungaji bora.
Timu ya Kilimani ambayo imeshika nafasi ya pili imenyakua Shilingi Milioni Moja (1,000,000) kwenye Fainali hiyo iliyofanyika Alhamisi Usiku wa Aprili 20, 2023, katika Kiwanja cha Alabama, Jimbo la Kikwajuni, mjini Unguja, Zanzibar.
Kwa upande wake, Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi ambaye ndiyo Mbunge wa Jimbo hilo, Mhandisi Hamad Masauni alisema Mashindano hayo ni muhimu jimboni humo na yataendelea kufanyika kwa kuwa yanaleta umoja.
Pia alitangaza kuwa, Uwanja huo uliofanyika fainali hiyo unatarajiwa kujengwa na kuwa wa kisasa ili kukuza vipaji vya michezo vya wananchi wa jimbo hilo.