NA MWANDISHI WAF
WAKAZI wa Mbarali wameipongeza Serikali kupitia Wizara ya Afya na wadau wa huduma za macho kwa kuwapatia matibabu ya macho bila malipo.

"Mimi nilifanyiwa macho yote mawili yalikuwa na mtoto wa jicho na hadi sasa naendelea vizuri.Tunaishukuru Serikali kwa kutupatia huduma sisi watu wa chini,huduma hizi ni bila malipo ninashukuru sana."

Amesema, mara baada ya kupata tatizo hilo alikua akinunua dawa kwenye maduka bila ushauri wa madaktari "nawashauri wananchi wasijinunulie dawa mje moja kwa moja kwani madaktari wapo na huduma ni nzuri".

"Tunamshukuru Mama kwa kutusaidia mambo mengi kama barabara,ametuletea mbolea,natoa sifa kwa Dkt. Samia anatuhudumia sisi watu wa hali hii kwani habagui na hachagui."
Kambi ya upasuaji wa mtoto wa jicho wilayani Mbarali imeanza tarehe 11 Aprili,2023 na inatarajiwa kumalizika tarehe 20 Aprili,2023.Inaratibiwa na Wizara ya Afya kwa kushirikiana na Shirika la Hellen Keler International la hapa nchini.