Wakuu wa mikoa wapigwa msasa biashara ya hewa ukaa

NA OR-TAMISEMI

WAKUU wa mikoa yote Tanzania Bara wamepewa elimu juu ya biashara ya hewa ukaa nchini ambayo itasaidia kuongeza mapato na kuimarisha utoaji wa huduma kwenye mamlaka za Serikali za Mitaa.

Hayo yameelezwa Aprili 3, 2023 jijini Dodoma katika kikao cha pamoja kilichopngozwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR-TAMISEMI),Mhe. Angellah Kairuki na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira, Dkt. Selemani Jafo.

Akizungumza katika kikao hicho, Mkurugenzi wa Mazingira kutoka Ofisi ya Makamu wa Rais, Dkt. Andrew Komba amesema biashara ya kaboni ni uwezo wa msitu wa Kitropiki au Asili kunyonya tani za hewa ukaa ambapo sisi ni alama katika utunzaji wa mazingira yaani Kaboni Credit.

Amesema, utunzaji wa misitu mikubwa unawezesha kunyonya hewa ya kaboni kwenye hewa, hivyo kupunguza athari kwenye tabaka la ozone ambalo linaathirika kutokana na msongamano wa hewa ya ukaa linalosababishwa na uwepo wa viwanda vikubwa duniani, matumizi ya magari yanayotumia Petroli na Diseli, pamoja na matumizi ya kuni na uchafuzi mwingine wa mazingira.

Amesema, biashara ya Kaboni ina masoko ya makubwa ya aina mbili yaani soko la hiari pamoja na Soko la Umoja wa Mataifa ambalo ni lazima kwa wenye viwanda vikubwa duniani kuhakikisha wanatunza mazingira kwa kulipia misitu inayosaidia kupunguza hewa ukaa.

Naye Afisa Mazingira kutoka Ofisi ya Rais-TAMISEMI, Bi.Hawa Mwechaga amesema, kati ya vijiji vilivyonufaika na biashara ya hewa ukaa ni Halmashauri ya Wilaya ya Tanganyika ambapo kwa mwaka wanapata zaidi ya shilingi Bilioni 7 ambazo zinawasiaida katika utekelezaji wa miradi ya maendeleo.

Kwa sasa kanuni zimeshaandaliwa ambazo sitasimamia biashara hii ya ukaa kwenye Mamlaka za Serikali za Mitaa.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news