NA DIRAMAKINI
MATAIFA ya Kigeni yamewahamisha wanadiplomasia, wafanyakazi na wengine kutoka Sudan siku ya Jumapili wakati mapigano yakidumu kwa siku tisa bila dalili ya makubaliano kusitisha hali hiyo ambayo yalikuwa yametangazwa kwa ajili ya sherehe za Eid El Fitr kwa Waislamu.
Wanajeshi wa Ufaransa wakishirikiana kupakia mali za watu waliohamishwa, kwenye ndege katika uwanja wa ndege wa Khartoum nchini Sudan, Jumapili, Aprili 23, 2023. (Picha na AP)
Kwa mujibu wa AP, wakati mataifa yenye nguvu duniani kama Marekani na Uingereza yakiwasafirisha kwa ndege wanadiplomasia wao kutoka mji mkuu wa Khartoum, Wasudan walitaka sana kukimbia machafuko hayo. Wengi walionekana wameamabatana barabarani ili kuvuka mpaka wa Kaskazini kuingia Misri.
"Familia yangu, mama yangu, kaka zangu na wapwa zangu wako njiani kutoka Sudan kwenda Cairo kupitia Aswan," mtayarishaji filamu maarufu wa Sudan Amjad Abual-Ala aliandika kwenye ukurasa wake wa Facebook.
Mapigano yalipamba moto huko Omdurman, mji ulio ng'ambo ya Mto Nile kutoka Khartoum, wakaazi walisema, licha ya matarajio ya kusitisha mapigano katika sikukuu ya Eid al-Fitr mambo hayakuwa hivyo.
"Hatukuona suluhu kama hiyo," Amin al-Tayed alisema kutoka nyumbani kwake karibu na makao makuu ya Televisheni ya serikali huko Omdurman, akiongeza kuwa milio ya risasi na milipuko ya mabomu ilitikisa jiji hilo.
Zaidi ya watu 420, wakiwemo raia 264, wameuawa na zaidi ya 3,700 kujeruhiwa katika mapigano kati ya jeshi la Sudan na kundi lenye nguvu la kijeshi linalojulikana kama Rapid Support Forces (RSF).
RSF ilisema vikosi vya jeshi vilianzisha mashambulizi ya anga kwenye kitongoji cha Kafouri, Kaskazini mwa Khartoum. Hakukuwa na maoni yoyote ya jeshi.
Vurugu zinazoendelea zimeathiri shughuli katika uwanja mkuu wa kimataifa wa ndege, kuharibu shughuli za usafiri wa ndege huku viwanja vingine vikisitisha kutoa huduma.
Mkuu wa Sera za Kigeni wa Umoja wa Ulaya, Josep Borrell alituma ujumbe kwenye mtandao wa kijamii wa Twitter akisema kuwa, alikuwa amezungumza na makamanda hasimu, akiwataka kusitishwa mara moja mapigano ili kuwalinda raia na waweze kuwahamisha raia wa Umoja wa Ulaya.
Katika mapigano mengine, afisa mkuu wa kijeshi alisema walizuia shambulio la RSF kwenye Gereza la Kober huko Khartoum ambapo mtawala wa muda mrefu wa Sudan, Omar al-Bashir, na maafisa wa zamani katika harakati zake wameshikiliwa tangu kuondolewa kwake 2019.
Afisa huyo, ambaye hakutaka kutajwa jina lake kwa sababu hakuruhusiwa kuzungumza na vyombo vya habari, alisema idadi kubwa ya wafungwa walikimbia, lakini al-Bashir na wafungwa wengine mashuhuri walikuwa katika eneo "salama sana", na kuongeza kuwa "wachache wafungwa” waliuawa au kujeruhiwa.
RSF ilidai kuwa, wanajeshi walimwondoa al-Bashir na wafungwa wengine katika kituo hicho, ingawa taarifa hiyo haikuweza kuthibitishwa kwa kina.
Kivuko cha mpaka cha Arqin na Misri kilikuwa kimejaa takribani mabasi 30 ya abiria ya watu wasiopungua 55 kila moja, alisema Suliman al-Kouni, mwanafunzi wa Misri ambaye alitorokea Kaskazini kutoka Khartoum na makumi ya wanafunzi wengine.
"Tulisafiri kwa saa 15 kwenye ardhi huku tukiwa na hofu ya usalama wetu," al-Kouni aliambia Associated Press kwa simu. "Lakini wengi wa marafiki zetu bado wamenasa nchini Sudan."
Pia, iliripotiwa kuwa Sudan ilikaribia "kukaribia kuporomoka" kwa huduma za intaneti na simu Jumapili, kulingana na huduma ya ufuatiliaji NetBlocks.
"Inawezekana kuwa miundombinu imeharibiwa au kuharibika,"Mkurugenzi wa Netblocks, Alp Toker alisema. "Hii itakuwa na athari kubwa kwa uwezo wa wakaazi kukaa salama na itaathiri mipango ya uokoaji inayoendelea,"amefafanua. (AP)