NA DIRAMAKINI
WAKENYA wameshauriwa kufunga mikanda yao kwa muda wa miaka miwili ijayo kabla ya mikakati inayotekelezwa na utawala wa sasa kuanza kuzaa matunda, kwani kuna matumaini.
Mheshimiwa Musalia Mudavadi ambaye ni Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Kenya ameyabainisha hayo kwa wabunge wa Bunge la Kitaifa huku akibainisha hakuna suluhu ya haraka kwa changamoto zinazoikumba nchi.
Akizungumza wakati akijibu maswali kutoka kwa wabunge hao, Mudavadi alisema Serikali ya Kenya Kwanza imeweka mikakati ya kujaribu kukabiliana na gharama za juu za maisha, ikiwa ni pamoja na kuanzisha msamaha wa ushuru wa bidhaa za chakula zenye thamani ya shilingi bilioni 10 za Kenya na kuwataka wanaonufaika nazo kuifikisha kwa Wakenya wenzao.
Waziri Mkuu huyo pia alisema, Serikali imeandaa mkakati mahususi ambao utasaidia kupunguza gharama ya mafuta katika siku za usoni.
Alipoulizwa ni lini Wakenya wataanza kufurahia hatua ambazo zimewekwa, Waziri Mkuu Mudavadi alisisitiza kwamba haitakuwa hivi karibuni.
"Ninataka kuwa mwaminifu sana kwa Bunge hili na kwa watu wa Kenya, kwamba tuko katika hili kwa muda mrefu, hali ambayo tuko nayo haiwezi kutamanika kama kahawa ya papo hapo.
"Tutazingatia vipaumbele na kuvifanya kuwa endelevu...na tunahitaji kuwa tayari kuwa na angalau miaka miwili ya kuzipatia ufumbuzi changamoto, lakini kuna matumaini,"alisema.
Mheshimiwa Mudavadi akijibu swali lililowasilishwa na Kiongozi wa Wengi Kimani Ichung’wah, pia alibainisha kuwa, Serikali ya Kenya Kwanza haitapuuza uamuzi wao wa kutotoa ruzuku ya matumizi.
"Hatuwezi kwa dhati kabisa kuendeleza ruzuku ya matumizi, kama taifa tunapaswa kuwa waaminifu kwetu wenyewe. Wakati kulikuwa na ruzuku ya mafuta, ilikuwa ikigharimu serikali ya Kenya shilingi 16 bilioni za Kenya hadi shilingi 20 bilioni kwa mwezi, ambayo haikuwezekana kuendelezwa, bila kujali ni serikali gani inayoongoza, sio jawabu,"alibainisha.
Waziri Mkuu hata hivyo alisema ruzuku ya mbolea itaendelea zaidi ya msimu huu huku serikali ikijaribu kuongeza uzalishaji baada ya kushuhudia mavuno machache zaidi ya mahindi katika kipindi cha miaka 10 iliyopita kutokana na ukame.
Amesema kuwa uongozi utaendelea kuagiza nafaka kutoka nje ili kukidhi mahitaji yaliyopo, ingawa msamaha wa ushuru umepangwa kukamilika ifikapo Agosti ili mahindi yanayoagizwa kutoka nje yasisababishe kikwazo baada ya wakulima kuvuna nchini.