NA JOSEPH MAHUMI-WFM
WIZARA ya Fedha na Mipango imesema inatambua na kuthamini mchango mkubwa wa waandishi wa habari katika kuuhabarisha umma kusuhu Sera, Mipango, na Mikakati mbalimbali inayotekelezwa na serikali kupitia wizara hiyo.
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Fedha na Mipango Bw. Benny Mwaipaja akizungumza wakati akifungua Semina elekezi kwa wahariri wa vyombo mbalimbali vya habari iliolenga kuwajengea uelewa wa masuala mbalimbali yanatokelezwa na Wizara ya Fedha na Mipango, katika ofisi ndogo ya Hazina, jijini Arusha.
Hayo yamesemwa Jijini Arusha na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Benny Mwaipaja, wakati akifungua semina elekezi kwa baadhi ya wahariri wa vyombo vya habari nchini, iliyolenga kuwajengea uelewa wa masuala mbalimbali yanayotekelezwa na Wizara ya Fedha na Mipango.
Mhasibu Mkuu wa Kitengo cha Pensheni, Wizara ya Fedha na Mipango Bi. Eugene Jairo akizungumza wakati akiwasilisha mada kuhusu Pensheni na Mafao baada ya kustaafu kwa wahariri wa vyombo mbalimbali vya habari waliohudhuria semina elekezi ya kuwajengea uelewa wa masuala mbalimbali yanatokelezwa na Wizara ya Fedha na Mipango, katika ofisi ndogo ya Hazina, jijini Arusha.
“Wananchi na umma wa watanzania kwa ujumla hawawezi kupata habari, Wizara inafanya nini, serikali inatekeleza nini bila ya ninyi na wadau wengine wa vyombo vya habari ambao hawako hapa,"alifafanua Bw.Mwaipaja.
Mhariri wa Gazeti la Nipashe, Bi. Salome Kitomari akichangia jambo wakati wa Semina elekezi kwa wahariri wa vyombo mbalimbali vya habari iliyoandaliwa na Wizara ya Fedha na Mipango kwa ajili ya kuwajengea uelewa wahariri kuhusu masuala mbalimbali yanatokelezwa na Wizara ya Fedha na Mipango, katika ofisi ndogo ya Hazina, jijini Arusha.
“Kama ambavyo Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, alivyoelekeza Wizara na Idara za Serikali kuwaambia wananchi mambo muhimu ambayo serikali inatekeleza, Sisi kama wizara tuna mambo mengi ya kuwaambia wananchi ikiwemo kuandaa Bajeti Kuu ya Serikali, namna tunavyotafuta rasilimali fedha kwa ajili ya kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo ambayo mmeiona ikiendelea kutekelezwa bila kukwama hii ni kwa sababu ya kazi kubwa inayofanywa na Wizara ya Fedha na Mipango,”alisema Mwaipaja.
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Fedha na Mipango Bw. Benny Mwaipaja (Katikati aliyekaa), Mwenyekiti wa Wahariri ambao wanaandika habari za Wizara ya Fedha kutoka Azam Media Group Bw. Ben Mwang'onda (Kulia aliyekaa) na Katibu wa Wahariri ambao wanaandika habari za Wizara ya Fedha kutoka Clouds Media Group Bi. Joyce Shebe wakiwa katika picha ya Pamoja na wahariri mbalimbali baada ya ufunguzio wa semina elekezi kwa wahariri hao iliyoandaliwa na Waziri wa Fedha na Mipango kuhusu masuala mbalimbali yanatokelezwa na Wizara ya Fedha na Mipango, katika ofisi ndogo ya Hazina, jijini Arusha.
Semina hiyo ni moja ya njia za kimkakati katika utekelezaji wa Mkakati wa Wizara wa Mawasiliano (Communication Strategy) ambapo Wizara inakutana na wadau mbalimbali wakiwemo waandishi wa habari. Miongoni mwa mada zitakazowasilishwa ni utekelezaji wa Bajeti ya 2022/2023 na Mwelekeo wa Bajeti Kuu ya Serikali, Utekelezaji wa Sheria ya Ubia kati ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi (PPP),muongozo wa utoaji mafao na pensheni kwa wastaafu na utekelezaji wa Malengo ya Maendeleo Endelevu (SDGs).