NA DIRAMAKINI
ASKARI Polisi kutoka Jeshi la Polisi Tanzania wanatarajia kupata mafunzo nchini Korea ikiwa ni utekelezaji wa makubaliano ya ushirikiano baina ya Shirika la Ushirikiano wa Kimataifa la Serikali ya Korea (KOICA) na Jeshi la Polisi Tanzania.
Hayo yamebainishwa leo Mei 9, 2023 Jijini Dar es Salaam na Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IJP Camillus Wambura wakati wa hafla ya kusaini makubalinao ya ushirikiano wa miaka mitatu wenye lengo la kushirikiana katika nyanja mbalimbali.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mkaazi wa KOICA Tanzania Manshik Shin alisema ushirikiano huo ni mwendelezo wa ushirikiano uliodumu kwa miaka mingi baina ya Korea Kusini na Tanzania.
Naye Balozi wa Korea Kusini Sunpyo Kim alisema Jeshi la Polisi Tanzania limekuwa likifanya vizuri katika kutekeleza majukumu yake.
Hafla hiyo pia ilihudhuriwa na Makamishna wa Polisi, Mwakilishi kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Maofisa kutoka Ubalozi wa Korea na KOICA.