NA DIRAMAKINI
MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam, CPA Amos Makalla ametangaza kuanza kwa awamu ya pili ya kampeni ya SAFISHA PENDEZESHA DAR ES SALAAM baada ya awamu ya kwanza ya kampeni hiyo iliyodumu kwa mwaka mmoja na miezi mitano kuwa na mafanikio makubwa ikiwemo kufanya Jiji hilo kushika nafasi ya sita kwa usafi Afrika.

Aidha, CPA Makalla amesema miongoni mwa mambo yayopaswa kuwekewa mkazo zaidi ni udhibiti wa ufanyaji biashara holela, usafishaji mazingira, upendezeshaji na upandaji miti kwenye bustani.
Kutokana na mwamko mkubwa wa usafi uliopo, RC Makalla ameelekeza kila halmashauri kushirikiana na wadau ambao wapo tayari kupendezesha Jiji huku akielekeza taasisi za TANROADS, TARURA na DAWASA kufanya kazi kwa ushirikiano.

Hata hivyo, RC Makalla ameendelea kusisitiza Wananchi kufanya usafi Kila ifikapo jumamos ya mwisho wa Mwezi huku akiwataka wafanyabiashara kufanya biashara kwenye maeneo waliyopangwa.