Balozi wa Marekani aiomba radhi Afrika Kusini

NA DIRAMAKINI

BALOZI wa Marekani nchini Afrika Kusini, Reuben Brigety, ameiomba radhi Serikali ya Afrika Kusini baada ya kuituhumu nchi hiyo kwa kuiuzia Urusi silaha.
Mkutano kati ya Balozi wa Marekani nchini Afrika Kusini, Reuben Brigety na Waziri wa Uhusiano wa Kimataifa na Ushirikiano, Mheshimiwa Naledi Pandor ambao umefanyika Mei 12, 2023 jijini Pretoria.(Picha na Twitter/@DIRCO_ZA).

Brigety aliitwa kwenye mkutano wa Ijumaa mchana na Waziri wa Uhusiano wa Kimataifa na Ushirikiano, Mheshimiwa Naledi Pandor.

Wizara ya Mambo ya Nje inasema Brigety alikiri kwamba alivuka mipaka kwa kushindwa kufuata njia za kidiplomasia zilizowekwa ili kuwasilisha matatizo ya nchi yake.

Kwa mujibu wa wizara hiyo, Afŕika Kusini inajulikana kwa kuwa na mchakato thabiti na mkali zaidi wakati wa kuuza silaha kwa nchi nyingine.

Leo Jumamosi, wajumbe maalum wa Rais Cyril Ramaphosa, wakiongozwa na Sydney Mufamadi, watatoa taarifa kwa wanahabari kuhusu ziara yao ya hivi karibuni nchini Marekani.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news