NA DIRAMAKINI
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi,Mheshimiwa Dkt.Hussein Ali Mwinyi leo ametembelewa na Balozi wa Norway nchini, Mhe. Elisabeth Jacobsen aliyefika Ikulu kumuaga baada ya kukamilisha kipindi chake cha miaka mitano akiiwakilisha nchi yake hapa Tanzania.

Balozi Elisabeth baada ya kuhudumu Tanzania kwa muda wa miaka hiyo anarejea Norway akiwa mstaafu.