NA DIRAMAKINI
YANGA SC ya jijini Dar es Salaam imeitangaza Kampuni ya Berger Paints International inayotengeneza rangi za Robbialac kuwa mshirika wake ambaye atafanya kazi ya kupaka rangi jengo lao la makao makuu lililopo Jangwani jijini Dar es Salaam.
Akizungumzia kuhusu hatua hiyo,Mkurugenzi wa Fedha na Utawala wa Yanga, CPA Haji Mfikirwa amesema kuwa, “Katika kutekeleza ahadi ya Rais wa Yanga Engenier Hersi Said ya kuboresha miundombinu ya klabu, leo tunaitangaza Kampuni ya Berger International inayotengeneza rangi za Robbialac kama mshirika wetu ambaye atafanya kazi ya kupaka rangi jengo letu hapa makao makuu ya Yanga ‘Jangwani’.
"Pia kwa mashabiki wa Yanga wenye kadi ya mwanachama au Shabiki wa Yanga watapata punguzo la bidhaa za Robbialac,”amesema Haji Mfikirwa
Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu Berger Paints, Salim Bharwan amesema,“Tunaamini Yanga imekuwa ikifanya vizuri ndani na nje ya nchi, tunayo furaha kufanya kazi nao sisi kama Kampuni ya Berger Paints na tunayofuraha kuzindua kampeni yetu iitwayo Mwaga Rangi Uipendayo.
"Na kipekee kabisa tunayo slogan nyingine ya Mwaga Rangi na Yanga,"amefafanua Mkurugenzi Mkuu wa Berger Paints, Bw.Salim Bharwan.