BREAKING NEWS: Rais Dkt.Samia ateua mabalozi mbalimbali

NA GODFREY NNKO

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan amefanya uteuzi wa mabalozi mbalimbali.

Hayo ni kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo Mei 22, 2023 na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu, Bi.Zuhura Yunus.

Mosi, Mheshimiwa Rais Dkt.Samia amemteua Meja Jenerali Ramson Godwin Mwaisaka kuwa Balozi. Kabla ya uteuzi huo, Meja Jenerali Mwaisaka alikuwa Mkuu wa Kamandi ya Jeshi la Wanamaji (JWTZ).

Pili,amemteua Meja Jenerali Paul Kisesa Simuli kuwa Balozi. Kabla ya uteuzi huo Meja Jenerali Simuli alikuwa Mkuu wa Utumishi Jeshini (JWTZ).

Tatu, amemteua Bw. Mohamed Awesu kuwa Balozi. Kabla ya uteuzi huo Bw. Awesu alikuwa Konseli Mkuu, Konseli ya Tanzania, Jeddah Saudia Arabia.

Nne, amemteua Bw. Gelasius Byakanwa kuwa Balozi. Kabla ya uteuzi huo Bw. Byakanwa alikuwa Afisa Mkuu Ubalozi wa Tanzania, Korea ya Kusini.

Tano,amemteua Dkt. Mohamed Juma Abdallah kuwa Balozi. Kabla ya uteuzi huo Dkt. Abdallah alikuwa Katibu Tawala Mkoa wa Kaskazini Unguja.

Sita,amemteua Bw. Hassan Mwamweta kuwa Balozi. Kabla ya uteuzi huo Bw. Mwamweta alikuwa Afisa Mambo ya Nje Mwandamizi na Mkuu wa Utawala, Ubalozi wa Tanzania, Uturuki.

Saba,amemteua Bw. Imani Salum Njalikai kuwa Balozi. Kabla ya uteuzi huo Bw. Njalikai alikuwa Afisa wa Mambo ya Nje Mkuu na Msaidizi wa Waziri Mkuu – Hotuba

Nane,amemteua Bw. Khamis Mussa Omar kuwa Balozi. Kabla ya uteuzi huo Bw. Mussa alikuwa Kaimu Mwakilishi wa Kudumu, Ubalozi wa Tanzania Ufaransa.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, uteuzi huu wa Mabalozi umeanza tarehe 10 Mei, 2023 na wataapishwa kwa tarehe itakayopangwa baadae.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news