NA MWANDISHI WETU
JUMUIYA ya Wahariri Afrika Mashariki imemchagua Daniel Kalinaki wa Jukwaa la Wahariri Uganda kuwa Rais wa Jumuiya ya Wahariri Afrika Mashariki kuanzia Mei 12, 2023, ambapo ataongoza kwa mwaka mmoja.

Deodatus Balile, ambaye ni
Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF), naye amechaguliwa kuwa
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wahariri Afrika Mashariki, kuanzia Mei, 2024
hadi Mei, 2025.
Kwa mujibu wa Katiba ya Jumuiya ya Wahariri Afrika Mashariki, katika kipindi cha mwaka mmoja ambacho Balile anasubiri kushika wadhifa wa Urais wa Jumuiya ya Wahariri Afrika Mashariki mwezi Mei 2024, kwa sasa atakuwa ni Naibu Rais wa Jumuiya ya Wahariri ya Afrika Mashariki.