NA GODFREY NNKO
MAMLAKA ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA) imesema mtu aliyeathiriwa afya ya akili kwa matumizi ya dawa za kulevya anakuwa ameathirika upande wa fikra, upande wa hisia na tabia.
Hayo yamebainishwa leo Mei 11, 2023 na Kamishna Jenerali Msaidizi wa Kinga na Huduma za Utangamano kutoka DCEA, Dkt.Cassian Nyandindi wakati akizungumza katika kipindi cha Supa Breakfast cha East Africa Redio jijini Dar es Salaam.
"Kama nilivyozungumza hapo awali, mtu anapokuwa na tatizo la afya ya akili maana yake anakuwa ameathirika katika mfumo wa fahamu hasa ubongo,na vitu ambavyo vinaathirika zaidi ni vitu vitatu,anakuwa ameathirika upande wa fikra, upande wa hisia na anakuwa ameathirika pia upande wa tabia.
"Sasa, fikra na hisia ndiyo vitu ambavyo haviwezi kuonekana kwa macho, huwezi kujua fikra ya mtu au hisia yake,hadi yeye mwenyewe akae aanze kuongea, lakini tabia ni kitu ambacho kinaonekana kwa macho na hicho ndiyo kitu ambacho watu mara nyingi wanakuwa wanakiona.
"Sasa nikianza kuzungumzia kwa upande wa tabia mara nyingi mtu anakuwa anfanya tabia ambazo hazikubaliki katika ile jamii ambayo inamzunguka na anashindwa kutimiza majukumu yake.
"Majukumu ambayo jamii inamtegemea aweze kuyafanya,mfano tu unaweza akawa anafanya tabia ambazo kama anaongeaongea peke yake, alikuwa nadhifu, ghafla anabadilika anakuwa mchafu,hapo unakuta ameanza tabia ya udokozi na wizi kwa hiyo anafanya zile tabia ambazo hazikubaliki katika jamii ambayo inamzunguka.
"Unaweza ukamkuta pia labda amekaa peke yake anahangaika, labda anajikuna au anatoa wadudu kwenye ngozi, ukimuuliza bwana kuna kitu gani kinakutembelea, wewe hauoni kitu chochote, lakini atasema labda kuna wadudu ambao wanamtembelea au anapiga kelele aua anaongea na watu ambao usiowaona au analalamika kuna vitu ambavyo vinamtokea.
"Mwingine anashindwa kupata usingizi, kwa hiyo ni zile tabia ambazo hazikubaliki katika jamii ndiye yeye anakuwa anazionyesha, tunaanza kuona sasa hapa kuna tatizo la akili na kuna kitu ambacho hakipo sawa sawa.
"Sasa kwa upande wa hisia, wengi wao unaweza kumkuta labda yupo katika hali ya huzuni muda mwingi au anakuwa katika hali ya wasiwasi na ukimuuliza mara nyingi anakuwa ana sababu ya msingi, kwa nini anajisikia hivyo, ndiyo maana kuna wachache inategemeana na sehemu ya ubongo ambayo imeathirika anaweza akawa na furaha iliyopitiliza kipimo.
"Unamuuliza mtu wewe una kitu gani leo unakifurahia,unakuta mtu hana sababu ya msingi, lakini anacheka tu peke yake. Kwa hiyo, ni vitu kama hivyo, kwa hiyo mambo ya msingi ni matatu ambayo nimeyasema kuna suala la hisia, kuna suala la fikra na kuna suala la tabia,"amebainisha Dkt.Nyandindi.

Tags
DCEA
DCEA Tanzania
Habari
Kataa Dawa za Kulevya na Timiza Ndoto Zako
Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA)