NA DIRAMAKINI
Dar es Salaam
RAIS mstaafu wa Awamu ya Nne wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete ameeleza kupokea kwa mshituko na huzuni kubwa taarifa ya kifo cha Mheshimiwa Bernard Kamillius Membe.
Hayo ameyabainisha Mei 12, 2023 kupitia taarifa iliyotolewa na Ofisi ya Rais mstaafu Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete iliyopo Kitalu Na.152 Barabara ya Haile Sellasie, Masaki jijini Dar es Salaam.
"Mama Dorcas Membe, salaam! Nimepokea kwa mshituko na huzuni kubwa taarifa ya kifo cha Mheshimiwa Bernard Kamillius Membe. Nimemfahamu miaka mingi, tumetoka nae mbali na tumesaidiana kwa mengi. Familia zetu, na mapito ya maisha yetu yamehusiana sana.
"Bernard Kamillius Membe alikuwa ni mtu wa msaada mkubwa kwangu katika maisha yangu ya kikazi na kisiasa. Nilimuamini na kumtumainia katika nafasi zote alizohudumu kwenye baraza langu la mawaziri. Aliwahi kuwa Naibu Waziri katika Wizara ya Mambo ya Ndani, na Wizara ya Nishati na Madini.
"Halikadhalika, aliwahi kuwa Waziri wangu wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa kwa miaka tisa ambapo alifanya kazi kubwa na nzuri ya kuendeleza maslahi ya Tanzania katika medani za Kimataifa;