Fanya mema hata kama umetendewa mabaya

NA ADELADIUS MAKWEGA

WAKRISTO wameambiwa kuwa wanalazimika kuishi vizuri na wenzao na kutenda mema hata kama wametendewa mabaya na mtu yoyote yule. Hayo yamesema na Padri Samwel Masanja, Paroko wa Parokia ya Malya, Jimbo Kuu Katoliki la Mwanza katika Kanisa la Bikira Maria Malkia wa Wamisionari.
“Unaweza kupitia changamoto mbalimbali,hata mateso lakini tunalazimika kutenda mema, si kulipa mabaya, tunalazikimika kuishi vizuri na si kuishi vibaya, wewe unapopitia changamoto mbalimbali unatakiwa kuchagua kutenda mema tu wala si kutenda mabaya. Kwa wale wenye nafasi mbalimbali wazitumie vizuri, je wewe ni kati ya hao wenye chanzo cha vurugu, wewe ni chanzio cha masengenyo ? Wanaopenda kulipa mabaya?” 

Akihubiri katika misa hiyo ya domika ya sita baada ya Pasaka ya Mwaka A wa Liturjia ya Kanisa, Paroko Masanja alisema kuwa nafasi mbalimbali tulizo nazo tusizitumie kuwanyanyasa wengine kwani kufanya hivyo ni kwenda kinyume na mapenzi ya Mungu. 
Misa hiyo pia iliyosindikizwa na nyimbo zilizoimbwa na Kwaya ya Mtakatifu Benedikt iliambatana na nia na maombi kadhaa, mojawapo ya maombi ya misa hii liilikuwa hili, 

“EE Bwana Yesu ulituahidi msaidizi baada ya kuondoka kwako, utasaidia kumtambua na kumpokea hili atuongoze katika maisha yetu ya kila siku, ee Bwana, twakuomba utusikie.” 

Mwishoni mwa misa hiyo iliyoanza saa 12.00 ya asubuhi ulifanyika mchango wa kumtemgemeza Mwalimu wa Kwaya ambapo kiasi cha fedha kinachokaribia laki nne kilichangiwa, baada mchango huo kukamilika Padri Masanja alimpa nafasi ya kushukuru mwalimu Pascal Clement, 
“Waamini wezangu, nawashukuru kwa kutoa sehemu za mali zenu kwa ajili ya kufanya uinjilishaji katika kwaya yetu, nia ni kusaidia kwaya hii kujikomboa katika kuifanya kazi ya kuinjilisha na kufanya hivyo kuna manufaa makubwa kwa Kanisa la Malya. Nawaombeni kila mmoja wetu pia aguswe kujiunga na kwaya yetu maana waimbaji wengi umri wao ni mkubwa, wanazeeka.” 

Hadi misa hiyo ya kwanza inamalizika, hali ya hewa ya eneo la Malya lililopo katika Wilaya Kwimba mkoani Mwanza kwa juma zima jua kali limetamalaki kwa siku sita, nayo mvua ikinyesha kwa siku moja tu na kuipoza ardhi ya eneo hili na kuendelea kuyajaza mabonde ambayo sasa yanavunwa mpunga. 
Mwandishi wa ripoti hii amebaini kuwa mara baada ya kuvumwa mpunga huo wa mwezi Mei uliopandwa kati ya Disemba 2022 na Januari 2023. Mvua kama hii iliyonyesha mara moja katika juma ina manufaa makubwa, inaitwa mvua ya kukuza machipukizi ya mpunga ambayo huwa mdogo wakati wa kuvunwa mwezi Mei na hukua vizuri ikifika mwezi Juni, Julai na Agosti wakulima huvuna mpunga wa mara ya pili wa machipukizi haya.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news