IJP mstaafu Balozi Simon Nyakoro Sirro aagwa rasmi jeshini

NA DIRAMAKINI

JESHI la Polisi Tanzania limemuaga rasmi leo Mei 10, 2023 aliyekuwa Mkuu wa jeshi hilo, IJP mstaafu Balozi Simon Nyakoro Sirro.

Ni baada ya kustaafu utumishi ndani ya Jeshi la Polisi Tanzania kwa mujibu wa sheria mwezi Machi, 2023 ambapo baada ya kuagwa, IJP mstaafu Sirro amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu, Dkt. Samia Suluhu Hassan, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi na Jeshi la Polisi kwa ujumla.

Sherehe za kumuaga IJP mstaafu Balozi Sirro zimefanyika katika Chuo chaTaaluma ya Polisi kilichopo Kurasini(DPA) jijini Dar es Salaam kwa gwaride maalum la kumuaga ikiwa ni utaratibu wa Jeshi la Polisi kuwaaga kwa gwaride maalum viongozi wa polisi waliofikia cheo cha Kamishna wa Polisi na Inspekta Jenerali wa Polisi.

Jeshi la Polisi limesema IJP Mstaafu Balozi Simon Nyakoro Sirro amelitumika Jeshi la Polisi kwa miaka 30 tangu Februari 19,1993 alipojiunga rasmi hadi kustaafu mwezi Machi, 2023 na ni Mkuu wa Jeshi la Polisi wa 10 kuliongoza Jeshi la Polisi tangu uhuru.

Kwa mujibu wa jeshi hilo, IJP mstaafu Balozi Sirro ameliongoza jeshi hilo kuanzia Mei 28,2017 hadi Julai 20, 2022 na kupata mafanikio makubwa kwenye mapambano dhidi ya uhalifu na wahalifu ikiwemo kukomesha vitendo vya mauaji yaliyokuwa yakitokea wilayani Kibiti mkoani Pwani na maeneo mengine pamoja na kupunguza uhalifu nchini.

Historia

Jeshi la Polisi la Tanzania lilianzishwa rasmi Agosti 25, 1919 kwa tangazo la Serikali la Kiingereza lililotoka Gazeti la Serikali No.Vol.1 No.21-2583 kwa wakati huo likaitwa Jeshi la Polisi Tanganyika.

Lakini jeshi lilianzishwa kisheria kwa Sheria ya uanzishajiwa Jeshi la Polisi ya mwaka 1939 (THE POLICE FORCE AND AUXILIARY SERVICES ACT OF 1939) PRINCIPAL LEGISLATION. Sheria hii ndiyo inatumika hadi sasa japo imekuaikifanyiwa marekebisho ya mara kwa mara.

Makao Makuu ya Jeshi hilo kulinga na natangazo hilo yalikuwa Wilayani Lushoto Mkoani Tanga chini ya uongozi wa Major S.T Davis.

Baadae Mwaka 1921 Kundi la Wakaguzi Polisi kutoka Ulaya lilifika nchini Tanganyika na kuanzisha Shule ya Mafunzo maalumu ya upolisi huko mkoani Morogoro ilikukidhi mahitaji yao na kuwana Askari wenye weledi wakutosha. Pamoja na kuwa na Askari weusi waliofunzu mafunzo lakini bado Askari hao walibaki na vyeo vya chini vya Kipolisi kwani vyeo vya juu vyote walipewa Askari Wazungu.

Jeshi la Polisi la kikoloni lilikuwa naWanaume pekeyao, hakuna mwanamke aliyepewa nafasi ya kujiungana Jeshi, siyotukwa Watanganyika hata Askari waki koloni wote walikuwa wanaume.

Mafunzo yalilenga kumpa Askari mbinu za kumkandamiza Mwafrika, kuwaminisha kuwa kila walichosema wakoloni ndicho sahihi, ukandamizaji na udhalilishaji kwa Mwafrika ulikuwa mkubwa na ndiyo ilichukua sehemu kubwa ya mafunzo kwa Askari wa Kikoloni.

Askari iwalifundishwa utii kwa viongozi wakikoloni na ukatili dhidi ya waafrika hasa viongozi wa kikoloni pamoja na machifu.

Lengo lilikuwa ni kumtawala Mtanganyika kirahisi.Watanganyika alitumia silaha za jadi kukabiliana naAskari wa kikoloni, silaha hizo zilikuwa marungu, panga, mikuki, na mishare, pamoja na silaha zilizotengenezwa kwa mawe yaliyochongwa vyema.

Wakoloni waliona ni vyema waanzishe vituo vingi vya Polisi na mwaka 1925 Kituo cha kwanza rasmi cha Polisi nchini kilifunguliwa huko Lupa, TingatingaMbeya.

Mwaka 1930 MakaoMakuu yaPolisi yalihamishwa kutoka Lushoto Mkoani Tanga kwenda Dar es Salaam. Lengo lilikuwa kuwa na ngome imara ambayo ilisimamia utendaji wavituo vingin evyote vya Polisi, mawasiliano na maelekezo ya ninikifanyike vituo ni yalitolewa kila siku kwa vituo vyote vya Polisi. Radio na barua za kipolisi zilitumika kufikisha ujumbe vikosini.

Baadaye Mwaka 1949 kikosi cha kutulizaghasia, Motorized Company sasa Field Force Unit (F.F.U) kilianzishwa nchini na lengo la kikosi hicho ni kurejesha amani penye vurugu.

Vijana wa kitanganyika walianza kupinga ukandamizaji wamMkoloni dhidi yao, vijana hao waliongozwa na baadhi ya Askari waliotoka katika vita ya kwanza na ya pili ya Dunia.

Hivyo basi iliwalazimu wakoloni kuanzisha kikosi maalum cha kutulizaghasia, pia mwaka huo wa 1949 kwa kuzingatia weledi, Vijana mbalimbali wa Kiafrika tokas hule mbalimbali za Sekondari Tanganyika walichaguliwa kujiungana Jeshi la Polisi na kuwa Wakaguzi wa Polisi chini ya uangalizi wa muda maalum (Probation Inspectors).

Mwaka 1952 Kikosi maalum cha Mawasiliano (Signals Branch) kilianzishwaPolisi bila kutumia nyaya za simu. Lengo la kikosi hicho ni kuhakikisha Jeshi la Polisi lina wasiliana muda wote.

Mawasiliano yalisaidia kutoa na kusamba za taarifa kwa haraka zaidi na utekelezaji wake kufanyika na mwaka huo pia Askari wa kike (Women Police) walijiunga na Jeshi la Polisi chini ya uongozi wa Ms. Payee. Ms. Payee ndiye alikuwa kiongozi wa askari wa kike kwa kipindi hicho.

Mara tu baada ya Tanganyika kupata uhuru wake tarehe 9 Desemba 1961, Jeshi la Polisi lilianza kubadili mwelekeo wake toka katika kutumikia Wakoloni na kuanza kuwatumikia wananchi kwa mujibu wa sera za Serikali yaWananchi wa Tanganyika japo bado lilikuwa na mfumo wa kikoloni. Ilichukua muda kulibadilisha na kulifanya Jeshi la Polisi liwe la kumlinda Mtanganyika na mali zake.

Wakuu wa Jeshi la Polisi (IGP) toka Tanganyika had isasa.

Toka uhuru mpaka sasa Jeshi la Polisi limeongozwana Ma IGP kumi:-

Camillus M. Wambura (2022-sasa)
Simon N. Sirro (2017-2022)
Ernest J. Mangu (2014-2017)
Saidi A. Mwema. (2006 – 2013)
Omar I. Mahita. (1996 – 2006)
Haroun Mahundi (1984 -1996)
Solomon Lyaani (1980-1984)
Philemon N. Mgaya. (1975 – 1980)
Samweli H. Pundugu. (1973 – 1975)
Hamza Azizi (1970 – 1973)
Elangwa N. Shaidi (1964 – 1970),

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news