IJP Simon Nyakoro Sirro kuagwa leo baada ya kustaafu utumishi wa jeshi

NA DIRAMAKINI

JESHI la Polisi nchini limeandaa hafla maalum kwa ajili kumuaga aliyekuwa Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania, IJP mstaafu Balozi Simon Nyakoro Sirro baada ya kustaafu utumishi wa jeshi hilo.

Hayo ni kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa Mei 9, 2023 na msemaji wa jeshi hilo, David Misime ambapo ameeleza kuwa, sherehe za kumuaga Siro zitafanyika katika Chuo cha Taaluma ya Polisi Dar es Salaam (DPA) kilichopo Kurasini jijini Dar es Salaam leo Mei 10, 2023 kuanzia saa 1 asubuhi.

Taarifa hiyo imeeleza kutakuwa na gwaride maalum la kumuaga ikiwa ni utaratibu wa Jeshi la Polisi kuwaaga kwa gwaride maalum viongozi wa Polisi waliofikia cheo cha Kamishna wa Polisi na Inspekta Jenerali wa Polisi

IJP mstaafu Balozi Simon Nyakoro Sirro amelitumika Jeshi la Polisi kwa miaka 30 tangu Februari 19, 1993 alipojiunga rasmi hadi kustaafu mwezi Machi,2023 na ni Mkuu wa Jeshi la Polisi wa 10 kuliongoza jeshi hilo tangu uhuru na ameliongoza kuanzia tarehe Mei 28, 2017 hadi Julai 20, 2022.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news