Jela miaka 30 kwa kubaka mwanafunzi

NA DIRAMAKINI

MAHAKAMA ya Wilaya ya Kibaha mkoani Pwani imemuhukumu, Huseni Mapeo mkazi wa Kisabi huko Mlandizi kifungo cha miaka 30 jela baada ya kupatikana na hatia ya kumbaka mwanafunzi wa miaka 12 (jina linahifadhiwa).

Hukumu hiyo ya kesi ya jinai namba 09/2023 imetolewa Mei 11, 2023 na Mheshimiwa Hakimu Felister Ng’welu wa mahakama ya hiyo baada ya kusikiliza ushahidi wa pande zote.

Mheshimiwa Ng’welu alieleza kuwa, amejiridhisha kumtia hatiani mshitakiwa huyo kwa mujibu wa kifungu 130 (1), (2) (a) na kifungu 131 (1) cha kanuni ya adhabu sura ya 16 iliyofanyiwa marekebisho mwaka 2022.

Mtuhumiwa alitenda kosa hilo Septemba 25,2022 huko maeneo ya Kisabi,Wilaya ya Kipolisi Mlandizi Mkoa wa Pwani.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news