Jeshi la Polisi labisha hodi shuleni

NA DIRAMAKINI

MKAGUZI Msaidizi wa Jeshi la Polisi, Asha Mponda amewataka wanafunzi wa Shule ya Sekondari Namatula iliyopo Wilaya ya Nachingwea mkoani Lindi kutambua umuhimu wa elimu wanayoipata.

Mponda ameyasema hayo Mei 12, 2023 wakati alipokuwa akitoa elimu ya dawati la jinsia kwa wanafunzi hao shuleni hapo.

Amesema kuwa, elimu ni ufunguo wa maisha, hivyo kila mmoja anatakiwa kutambua kwamba mafanikio ya maisha yake ni elimu.

Akiwatolea mifano kadha wa kadha, aliwaambia ukiwaona polisi, madaktari, waalimu, mameneja wa kada mbalimbali, mawaziri, wote hao chimbuko lao ni elimu. Hivyo aliwasisitiza kusoma kwa bidii na kuishika elimu.

Mada nyingine alizowafundisha wanafunzi hao ni pamoja na kutambua haki na wajibu wa mtoto, jinsi ya kuepuka kufanyiwa vitendo vya ukatili, pamoja na athari za mapenzi ya jinsi moja.

Mbali na hayo, kufuatia maelekezo ya Maofisa wa Polisi Mkoa wa Morogoro kuhuishwa kwa Klabu Marafiki wa Polisi Shuleni, wakaguzi kata wa mkoa wa Morogoro wameitikia kwa vitendo maelekezo hayo kwa kuhuisha vikundi hivyo katika shule zilipo mkoani humo.

Vikiwa na lengo la kuwaweka karibu wanafunzi na Jeshi la Polisi kwa kutoa taarifa za vitendo vya ukatili vinavyoendelea kutokea kwenye shule mbalimbali na wanafunzi hao wawapo nyumbani.

Pia Jeshi la Polisi Mkoa wa Morogoro limesema kuwa, zoezi hilo ni endelevu huku lengo la zoezi hilo ni kuzifikia shule zote zilizopo mkoa huo wa Morogoro na kuhakikisha wanafunzi wanapata elimu hiyo na kuwajengea uwezo wa kutoa taarifa sahihi za vitendo vya ukatili wa kijinsia kwa Jeshi la Polisi.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news