Afisa Uuguzi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI), Ansila Makoi akimpima shinikizo la damu mkazi wa Manyara Tatu Isango aliyefika katika Hospitali ya Rufaa Mkoa wa Manyara (MRRH) kwa ajili ya kupatiwa matibabu ya moyo wakati wa kambi maalum ya siku tano inayofanywa na wataalam wa afya wa JKCI kwa kushirikiana na wenzao wa MRRH.
Daktari wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI),Magreth Ng’ondya akimsikiliza mkazi wa Manyara Liberan Assey aliyefika katika Hospitali ya Rufaa Mkoa wa Manyara (MRRH) kwa ajili ya kupatiwa matibabu ya moyo wakati wa kambi maalum ya siku tano inayofanywa na wataalam wa afya wa JKCI kwa kushirikiana na wenzao wa MRRH.
Afisa Lishe wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI), Husna Faraji akimsikiliza mkazi wa Manyara Bausi Nuru aliyekuwa anauliza swali kuhusu lishe bora wakati wa kambi maalum ya siku tano inayofanywa na wataalam wa afya wa JKCI kwa kushirikiana na wenzao wa MRRH.
Mtafiti wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI), Zabella Mkojera akimuuliza maswali ya ufahamu kuhusu magonjwa yasiyo yakuambukiza yakiwemo magonjwa ya moyo mkazi wa Manyara wakati wa kambi maalum ya siku tano inayofanywa na wataalam wa afya wa JKCI kwa kushirikiana na wenzao wa MRRH.(Picha na JKCI).