Madaktari bingwa wa magonjwa ya moyo kwa watoto wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) kwa kushirikiana na wenzao kutoka mradi wa Little Heart wa Shirika la Muntada Aid lenye makao yake makuu mjini London nchini Uingereza wakitanua Valvu ya moyo wa mtoto ambayo ilikuwa haipitishi damu vizuri wakati wa kambi maalum ya siku tano ya upasuaji wa moyo inayofanyika katika taasisi hiyo.
Madaktari bingwa wa magonjwa ya moyo kwa watoto wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) kwa kushirikiana na wenzao kutoka mradi wa Little Heart wa Shirika la Muntada Aid lenye makao yake makuu mjini London nchini Uingereza wakimfanyia mtoto kipimo cha kuangalia jinsi moyo unavyofanya kazi (Echocardiography) mara baada ya kumaliza kutanua Valvu ya moyo ambayo ilikuwa haipitishi damu vizuri wakati wa kambi maalum ya siku tano ya upasuaji wa moyo inayofanyika katika taasisi hiyo.
Madaktari bingwa wa upasuaji wa moyo kwa watoto wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) kwa kushirikiana na wenzao kutoka mradi wa Little Heart wa Shirika la Muntada Aid lenye makao yake makuu mjini London nchini Uingereza wakifanya upasuaji wa kuziba matundu mawili ya moyo wa mtoto wakati wa kambi maalum ya siku tano ya upasuaji wa moyo inayofanyika katika taasisi hiyo.(Picha na Hamisi Mussa).