NA MWANDISHI WETU
WMJJM
KATIKA kuadhimisha Siku ya Kimataifa ya Familia, Mei 15, 2023, Serikali kupitia Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum imezindua Kampeni ya Kitaifa ya Linda Maadili Sasa Rasmi kuhakikisha maadili yanalindwa na kuendana na mila na desturi za nchi.
Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Mhe. Dkt. Dorothy Gwajima akitembelea baadhi ya mabanda ya wajasiriamali na watoa huduma alipowasili katika viwanja vya Nyerere Square jijini Dodoma kwa ajili ya maadhimisho ya siku ya Kimataifa ya Familia Mei 15, 2023.
Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Mhe. Dkt. Dorothy Gwajima akizindua kampeni hiyo katika kongamano la maalum, amesema jamii yenyewe inatakiwa kuwajibika kwenye malezi yanayoendana na miiko na tamaduni za kitanzania ili kuimarisha familia na kuepuka mmomonyoko wa maadili.
Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Mhe. Dkt. Dorothy Gwajima akizungumza na wananchi wa mkoa wa Dodoma katika maadhimisho ya Siku ya Kimataiafa ya familia, viwanja vya Nyerere Square Mei 15, 2023.
Mhe. Dkt. Gwajima amebainisha kwamba takwimu za vitendo vya ukatili hasa kwa watoto zinaonesha asilimia 60 ukatili unafanyika nyumbani hivyo msingi wa kwanza katika kutelekeza kampeni hiyo ni kuanzia ndani ya familia.
Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Mwanaidi Ali Khamis akizungumza wakati wa kongamano la maadhimisho ya Siku ya familia jijini Dodoma, Mei 15, 2023.
"Bila maadili na upendo familia itakuwa ni kusanyiko la watu ambapo shetani anaweza kupitisha kusudi lake kwa urahisi badala ya kusudi la Mungu hivyo, kaeni vikao mtathmini maadili na upendo wenu, mkishindwa kupendana msipeleke athari kwa watoto mje ustawi wa jamii tuwape huduma,” amesema Mhe. Gwajima.
Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Mhe. Dkt. Dorothy Gwajima akizungumza na wananchi wa mkoa wa Dodoma katika maadhimisho ya Siku ya Kimataiafa ya familia, viwanja vya Nyerere Square Mei 15, 2023.
Kwa upande wake Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Dkt.John Jingu akieleza madhumuni ya Siku ya Kimataifa ya familia amebainisha kwamba siku hii ni Azimio la kimataifa lililofikiwa mwaka 1993 kupitia baraza la Umoja wa Mataifa.
Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Dkt..John Jingu akieleza lengo la maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Familia, wakati wa kongamano maalum lililofanyika jijini Dodoma Mei 15, 2023.
Dkt. Jingu ametoa wito kwa jamii kuitumia siku hii kutafakari na kuona namna gani familia zinatimiza jukumu la malezi na ustawi wake.
"Kaulimbiu ya Siku ya Kimataifa ya Familia, inatualika kuona umuhimu wa kuimarisha maadili na upendo katika familia zetu ili ziwe imara kwa manufaa ya jamii na Taifa kwa ujumla" amesema Dkt. Jingu.
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule akitoa salaam za mkoa wakati wa maadhimisho ya siku ya Kimataifa ya Familia Mei 15, 2023 jijini Dodoma.
Aidha, Mkuu wa Mkoa wa Dodoma amepongeza juhudi za Serikali kupitia Wizara ya Maendeleo ya Jamii,Jinsia ,Wanawake na Makundi Maalum kwa juhudi za kutoa za Elimuu juu ya umuhimu wa Familia na Upendo katika Jamii zetu.
Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Ustawi na Maendeleo ya Jamii, Mhe. Fatma Toufiq akieleza jambo katika kuadhimisha Siku y Kimataifa ya familia, jijini Dodoma Mei 15, 2023.
“Wizara ya Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wanawake na Makundi Maalum inafanya kazi nzuri sana kwani kauli mbiu ya “linda maadili “imesambaa sana katika jamii zetu na kumshawishi kila mmoja wetu kuwekeza katika Kulinda maadili na kupinga mmonyoko wa Maadili Nchini,”Rosemary Senyamule.
Wananchi waliojitokeza kwenye kongamano la maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Familia wakifuatilia matukio mbalimbali katika maahimisho hayo jijini Dodoma, Mei 15, 2023.
Baadhi ya wataalamu waliotoa mada katika maadhimisho hayo akiwemo mwanasaikolojia maarufu,Dkt. Chris Mauki amewakumbusha Wazazi kushiriki kikamilifu katika jukumu lao la Malezi kwani Jamii bora inajengwa na Utekelezaji wa majukumu kutoka pande zote mbili.
“Maadili yanaanza kuvunjika pale ambapo mmoja anashindwa kusimamia majukumua yake,Mtoto anachukua tabia asilimia 80 kutoka kwa wazazi na asilimia 20 kutoka nje.Wazazi tunakimbizana sana na pesa na kusahau kuwa walezi,"amesema Dkt. Mauki.