Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu), Dkt. Jim Yonazi akutana na kufanya mazungumzo na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakfu wa Mwalimu Nyerere Foundation (Mwalimu Nyerere Foundation), Bw. Joseph Butiku alipomtembelea ofisini kwake leo Mei 22, 2023 jijini Dodoma.
Wakfu wa Mwalimu Nyerere ulianzishwa mwaka 1996 na Hayati Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere ili kuendeleza urithi wake wa amani, umoja na maendeleo yanayozingatia watu.
Aidha, wakfu huo unalenga kufuatilia taasisi za umma na za kibinafsi na kutafuta mikakati ya kudumisha maadili yake ya uadilifu, usawa, na utawala wa sheria katika Afrika Mashariki na kwingineko.
Aidha, wakfu huo unalenga kufuatilia taasisi za umma na za kibinafsi na kutafuta mikakati ya kudumisha maadili yake ya uadilifu, usawa, na utawala wa sheria katika Afrika Mashariki na kwingineko.