NA DIRAMAKINI
JAMHURI ya Kenya imesema itazingatia eneo la kimkakati la Singapore, Kusini Mashariki mwa Asia kama lango la bidhaa zake.
Rais Dkt.William Ruto amesema hatua hiyo inaongozwa na dhamira ya Serikali ya kupanua masoko ya faida kwa mazao yake ya kilimo.
Amesema, Asia Kusini, inayoundwa na nchi 10 na yenye wakazi takribani milioni 670, inaipa Kenya soko la kipekee na kubwa la kuuza bidhaa zake.
Pia, amealika sekta binafsi ya Singapore kuwekeza katika sekta ya uchukuzi na usafirishaji ya Kenya ambayo inahitaji nguvu ya pamoja.

Aliyasema hayo hivi karibuni katika Ikulu ya Nairobi alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari akiwa na Waziri Mkuu wa Singapore, Lee Hsien Loong.
Awali, viongozi hao wawili walifanya mazungumzo baina ya nchi hizo mbili na kushuhudia kutiwa saini kwa Makubaliano kuhusu ICT, mabadiliko ya tabianchi na ukuzaji ujuzi.
Rais Ruto alisema makubaliano ya ICT yatarahisisha ushirikiano katika usalama wa mtandao, kuweka huduma za serikali kidijitali na kujenga uwezo wa ICT.
Alieleza kuwa MoU ya ukuzaji ujuzi itarahisisha ushirikiano katika kujenga uwezo wa rasilimali watu kwa watumishi wa umma na wanafunzi.
Waziri Mkuu alibainisha kuwa kutiwa saini kwa mkataba wa mabadiliko ya hali ya hewa kutajenga hatua ya pamoja ya kukabiliana na tishio kubwa zaidi lililopo kwa wanadamu.
"Uhusiano wetu umekuwa ukiongezeka. Tutaendeleza hili kwa kutafuta fursa zaidi za kiuchumi ambazo zitachochea ustawi wetu wa pamoja,”alisema Waziri Mkuu Loong.
Naibu Rais Rigathi Gachagua,Waziri Mkuu Musalia Mudavadi, Mwanasheria Mkuu Justin Muturi, mawaziri wa Mambo ya Nje Alfred Mutua, Teknolojia ya Mawasiliano (ICT) na Uchumi wa Dijitali Eliud Owalo, Utumishi wa Umma Aisha Jumwa, Wizara ya Mazingira, Mabadiliko ya Tabianchi na Misitu Saipan Tuya ni miongoni mwa viongozi wengine walikuwepo.