NA DIRAMAKINI
SERIKALI ya Jamhuri ya Kenya imesema kuwa, inawekeza katika uchumi wa kidijitali ili kuunda fursa zaidi za kiuchumi kwa vijana.
Mheshimiwa Rais Dkt.William Ruto amesema, Serikali imedhamiria kufanya hivyo kwa sababu ina nia ya kufanya Kenya kuwa kitovu cha uvumbuzi wa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) ili kufungua uwezo wa uchumi wa kidijitali.
Pia amesema, Serikali imeweka mikakati madhubuti kuhakikisha utekelezaji wa uchumi wa kidijitali unafanikiwa. Alitaja Sera ya Kitaifa ya TEHAMA, Sheria ya Kuanzisha Biashara ya Kenya, Sheria ya Kulinda Data, Mpango wa Uchumi wa Kidijitali na Sheria ya Matumizi Mabaya ya Kompyuta na Uhalifu wa Mtandao na mradi wa Konza Technopolis kuwa maeneo yanayoangaziwa.
"Ajenda ya mabadiliko ya kidijitali ni ya kweli, inawezekana na imejikita katika mfumo thabiti wa kitaasisi," alisema. Rais Ruto wakati akizungumza Alhamisi katika uzinduzi wa Fingo Africa inayoendeshwa na Ecobank katika Kituo cha Sarit jijini Nairobi.
Rais alisema, teknolojia ya kifedha itakuza ufanisi wa shughuli, kuimarisha usalama na kulinda data binafsi katika sekta ya fedha.