NA DIRAMAKINI
SERIKALI ya Jamhuri ya Kenya na Nigeria zimekubaliana kuimarisha uhusiano wa kidiplomasia na kibiashara.Rais wa Jamhuri ya Kenya, Mheshimiwa Dkt.William Ruto amesema kuwa, nchi hizo mbili zinajitahidi kuunda fursa zaidi kwa raia wao.
Rais alitaja kilimo, teknolojia, nishati mbadala na sekta ya huduma kuwa maeneo muhimu yenye maslahi kwa pande zote.
"Kenya ina nia ya kuongeza biashara na Nigeria. Tunatazamia kuongeza mauzo ya nje ya chai, mazao ya bustani, nguo na vyakula vilivyosindikwa.”
Rais Ruto alialika makampuni ya Nigeria kutafuta fursa nchini Kenya.Rais Ruto alisema hayo Jumapili alipokutana na Makamu wa Rais wa Nigeria, Prof Yemi Osinbajo katika Ikulu ya Nairobi.