NA DIRAMAKINI
JAMHURI ya Kenya imesema inathamini uhusiano mzuri wa kidplomasia na Uholanzi. Mheshimiwa Rais Dkt.William Ruto amesema hayo Jumatatu alipofanya mazungumzo na Willem-Alexander, Mfalme wa Uholanzi.
Viongozi hao wawili walijitolea kuimarisha uhusiano kati ya nchi hizo mbili kwa ustawi wa raia wao. Ikiwa ni pamoja na kuimarisha biashara ya kilimo cha bustani, mifugo, chai na kahawa, matunda, mboga mboga, samaki na tumbaku.
Rais Dkt.Ruto na Mfalme Alexander walijadili changamoto ya mabadiliko ya hali ya hewa, ajenda ya Kenya ya ukuaji wa kijani na uhifadhi wa wanyamapori.
Aidha, Serikali ya Uholanzi imesema itaendelea kusaidia Kenya katika kuendeleza ardhi kame,usambazaji wa maji na usafi wa mazingira vijijini, afya, maendeleo ya miundombinu na utafiti wa kilimo.