NA DIRAMAKINI
RAIS wa Jamhuri ya Kenya, Mheshimiwa William Ruto amesema,Serikali itawekeza katika elimu ili kuwawezesha vijana na kujenga nguvu kazi ambayo itasimamia maendeleo ya nchi.
Akizungumza hivi karibuni kwenye sherehe za miaka 100 ya Limuru Girls, Rais Ruto alisema serikali itatekeleza mageuzi ya elimu ili kuimarisha ubora.
"Mtaji wetu ni rasilimali yetu muhimu, lazima tuwekeze katika miundombinu ya shule ili kuinua ubora wa elimu ili tuwe na kizazi ambacho kiko tayari kuchukua fursa yao wakati utakapofika."
Rais alisema, serikali pia inawekeza katika teknolojia ya ICT, usindikaji wa mazao ya kilimo na nyumba za bei nafuu ili kutoa nafasi za kazi.
Rais Ruto aliongeza kuwa, anafanya kazi na kaunti kuanzisha maeneo ya ujumlishaji na viwanda ili kuimarisha biashara ya kilimo.
"Tuna mpango wa makusudi wa kukabiliana na ukosefu wa ajira na kuinua vijana wetu," alisema Mheshimiwa Rais Ruto.