NA DIRAMAKINI
VIJANA wa Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni jijini Dar es Salaam (KMC FC) wameibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Singida Big Stars kutoka mkoani Singida.
Ni kupitia mtanange wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara uliopigwa katika Dimba la Uhuru lililopo Halmashauri ya Manispaa ya Temeke jijini Dar es Salaam.
Mabao ya KMC yamefungwa na Daruwesh Saliboko dakika ya 20 akiunganisha pasi nzuri ya George Makang’a ambaye alikuwa karibu na eneo la hatari.
Bao la pili likiwekwa nyavuni na Cliff Buyoya dakika ya 84 akipokea pasi nzuri kutoka kwa mchezaji Steve Nzigamasabo.
Chini ya kocha mpya, Jamhuri Kihwelo (Julio) vijana hao wa Kindondoni maarufu kama Kino Boys wanafikisha alama 29 na kusogea nafasi ya 12 katika msimamo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara.
Aidha,Singida Big Stars kutoka mkoani Singida chini ya kocha Mholanzi, Hans van Pluijm wanabaki na alama 51 nafasi ya nne baada ya wote kucheza mechi 28 katika ligi hiyo yenye mvuto zaidi nchini.