Leo Mei 30, 2023 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi,Mheshimiwa Dkt.Hussein Ali Mwinyi anazungumza na Waandishi wa Habari kuanzia saa 4 kamili asubuhi Ikulu jijini Zanzibar ikiwa ni utaratibu aliojiwekea wa kuzungumza nao kila mwisho wa mwezi kuelezea mambo mbalimbali yanayohusiana na utekelezaji wa miradi ya maendeleo, ufumbuzi wa changamoto na mengineo. Pia, Mheshimiwa Rais Dkt.Mwinyi amekuwa akitoa nafasi ya kujibu maswali mbalimbali ya wanahabari;