Maafisa habari Wizara ya Mambo ya Ndani watakiwa kushirikiana

NA MWANDISHI WETU

KATIBU Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mheshimiwa Kaspar Mmuya amewataka Maafisa habari wa Wizara na vyombo vya Usalama vilivyopo wizara hiyo kushirikiana katika kuhabarisha na kuwaelimisha wananchi kuhusiana na mafanikio mbalimbali yanayopatikana.
Mheshimiwa Mmuya ameyasema hayo Mei 30, 2023 wakati akifungua mkutano wa mwaka na mafunzo kwa Wasemaji, Maafisa Habari, Mawasiliano na Uhusiano wa Wizara na Vyombo vyake vya usalama unaofanyika Jijini Dodoma.

Katibu Mkuu amebainisha kuwa jamii inatamani kusikia matukio mbalimbali yanayotekelezwa na Wizara hiyo, hivyo Maafisa hao wanaowajibu mkubwa wa kufanya kazi kwa pamoja kutoa taarifa kwa haraka na usahihi kwa kuzingatia weledi kuhusiana na kazi zinatotekelezwa na taasisi hizo.
Sambamba na hilo, pia amewataka kuwa na mawasiliano ya kimkakati kwa kujenga uhusiano mzuri baina ya jamii kupitia taarifa mbalimbali wanazozitoa hasa ikizingatiwa kuwa taasisi hizo zinafanya kazi moja kwa moja na wananchi.

Awali akimkaribisha mgeni Rasmi, Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Bi. Christina Mwangosi amesema lengo la mkutano huo ni kufanya tathmini ya pamoja kutokana na malengo ambayo walikua wamejiwekea.

Amefafanua kuwa katika mafunzo hayo watabadilishana uzoefu katika kutekeleza majukumu yao ya kazi.
Mkutano huo ambao unafanyika katika ukumbi wa Makao Makuu ya Magereza kuanzia Mei 30 hadi Juni 01, 2023 unawakutanisha Wasemaji, Maafisa Habari toka Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Jeshi la Polisi, Magereza, Uhamiaji, Zimamoto pamoja na NIDA.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news