Mke wa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mheshimiwa Dkt.Hussein Ali Mwinyi, Mama Mariam Mwinyi ambaye pia ni Mwenyekiti wa Taasisi ya Zanzibar Maisha Bora amekutana na Binti wa mtawala wa zamani wa Qatar, Sheikha Alanoud Hamad Al-Thani jijini Doha, Qatar.
Katika kikao hicho kwa pamoja walibadilishana mawazo juu ya ustawi wa wanawake na vijana hususani wanawake katika kujiendeleza kiuchumi, afya na elimu.
Sheikha amempongeza mama Mariam Mwinyi kwa kuanzisha Taasisi ya Zanzibar Maisha Bora ambayo imekuwa inapambana na unyanyasaji na ukatili wa kijinsia pamoja na kumwezesha mtoto wa kike katika masuala ya afya ya uzazi, kuwawezesha pia wanawake wanaojishughulisha na ukulima wa mwani.