NA MWANDISHI WETU
MKE wa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mheshimiwa Dkt.Hussein Ali Mwinyi, Mama Mariam Mwinyi,amewasihi wanadiaspora wanawake waishio nchini Qatar kuendeleza utaratibu wao wa kuleta mchango na shukrani nyumbani. Aidha, Mama Mariam Mwinyi amebainisha umuhimu wa kuwasaidia wanawake Zanzibar.
Mama Mariam Mwinyi ambaye pia ni Mwenyekiti wa Taasisi ya Zanzibar Maisha Bora ametumia nafasi hiyo kuwahutubia wanadiaspora wanawake walioko Qatar wakati wa sherehe za kutimiza mwaka mmoja tangu kuanzishwa kwa taasisi yake.
Wito huo unakuja kufuatia kuongezeka kwa kasi kwa wimbi la udhalilishaji, ambalo kwa kiasi kikubwa linaanzia katika ngazi ya familia.
Kwa upande wa wanadiaspora wamemuhakikishia Mama Mariam Mwinyi kuwa wataendelea kushirikiana naye katika jitihada zake za kuwahudumia wanawake, vijana na watoto nchini.