NA MWANDISHI WETU
MKE wa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapiunduzi, Mheshimiwa Dkt.Hussein Ali Mwinyi, Mama Mariam Mwinyi ambaye pia ni Muasisi na Mwenyekiti wa Bodi Zanzibar Maisha Bora Foundation amekutana na Mhe.Sheikha Moza bint Nasser, ambaye ni mama ya mfalme wa Qatar Tamir bin Hamad Al Thani na ni muasisi na mwenyekiti wa Qatar Foundation.
Mama Mariam Mwinyi alipata fursa ya kujadiliana na kubadilishana uzoefu juu ya kuimarisha jitihada mbalimbali za kuwainua kiustawi, kielimu na afya za wanawake, vijana na watoto.
Wakiwa katika mkutano huo Mei 24, 2023 Mhe.Sheikha Moza ameonesha nia ya awali ya kushirikiana na Mama Mariam Mwinyi kupitia ZMBF katika kuimarisha mikakati ya kupambana na ukatili na unyanyasaji wa kijinsia kwa wanawake, vijana na watoto Zanzibar.
Aidha, Mama Mariam amempongeza pia Mhe.Sheikha Moza kwa kujitolea kuwekeza katika sekta ya Elimu na Afya nchini Qatar na sehemu mbalimbali duniani na baadae kumkaribisha pia Zanzibar.
Awali, pia Mke wa Rais wa Zanzibar, Mama Mariam Mwinyi, ambaye pia ni Muasisi na Mwenyekiti wa Bodi Zanzibar Maisha Bora Foundation alikutana na uongozi wa Umoja wa Wanawake Qatar jijini Doha.
Katika mkutano huo, Mama Mariam Mwinyi alifafanua kuhusu taasisi yake na aina ya shughuli zinazofanywa na taasisi hiyo Zanzibar.